mimi nadhani tatizo ni uelewa wa vyama vya siasa ni nini na siasa ni nini , yawezekana kama sote tungeelewa hilo wao wasingesema na sisi tusingewashangaa.
vyama vya siasa ni makundi ya wanajamii ambao wameungana na kuachagua itikadi fulani au mifumo fulani ya kuongoza jamii.
sasa chama jukumu la kwanza ni kuwa na itikadi ili wanachama watambue sisi tunafuata nini?
lakini jukumu la pili la chama ni kutumia itikadi zao kutengeneza mpango wa maendeleo ya jamii.
hivyo katika uchaguzi chama kinasimamisha mtu kuwania nafasi ya uongozi akiongozwa na vitu viwili yaani itikadi na mipango.
kwa wananchi yapo mambo ambayo kamwe mtu yeye binafsi kamwe hawezi kuyakubali na atasema mimi jambo fulani silikubali hata iweje hivyo kama chama kinasema msimamo wake ni kitu fulani basi siwezi kukisapoti chama hicho maana nitakuwa nafanya hili jambo wanalolisapoti likue katika jamii yetu.
kwa bahati mbaya vyama vyetu hapa tanzania havina itikadi za kueleweka ambazo zinaweza kuwatofautisha na kutoa misimamo kwa wanachamai.
hivyo linabaki swala la mipango ya maendeleo.
kila uchaguzi unapofika kila chama kinatakiwa kutengeneza mpoango wake wa maendeleo ambao viongozi wake watautekeleza iwapo watapewa dhamana.
ni wajibu wa wananchi kuchambua mipango hii kila uchaguzi unapofika na kuchagua ule ambao wanaona unawapeleka katika maendeleo.
ni vibaya sana kwa wananchi kuchagua vyama mapema kwani unaondoa ushindani ambao huwasukuma vyama kutafuta mipango bora ya maendeleo ili kushawishi wananchi kuwapa nafasi.
wananchi kuchagua vyama mapema kunawaondoa vyama katika jukumu la msingi na kuingia katika kutengeneza mashabiki ambako kunaweza kukawa kwa kutumia njia ambazo hazileti maendeleo kwa wananchi.
kama tunataka maendeleo tujiweke katika kuchagua mipango ya maendeleo inayofaa, utekelezaji wa mipango, usimaiji wa mipango, usiamiaji wa watumishi na mengine na vyama vitambue kuwa haya sisi ndiyo tunayoyataka hivyo waanze kushindana kuyapanga haya.
Wanaosema imewazaa na imewalea