Elections 2010 CCM imepanga kusafirisha wanavyuo ambao ni wanachama kwenda kupiga kura

Elections 2010 CCM imepanga kusafirisha wanavyuo ambao ni wanachama kwenda kupiga kura

Mtz-halisi

Member
Joined
Nov 28, 2009
Posts
47
Reaction score
20
Habari niliyopata kama nusu saa iliyopita ni kuwa ccm imeandaa pesa za kujikimu kwa wanafunzi wote ambao ni wanachama wa chama hicho waende kupiga kura katika vituo vyao" naona ni ufisadi mkubwa unatendeka na ni kunyonga democrasia; inaumiza na kusikitisha kama haya mambo ni kweli.

Mungu atusaidie
 
Hata wafanyeje mwaka hue hawapiti
 
Mwenye macho ya kuona na aone!
Actuall Nia ya awali ya mpango huo ilikuwa ni hiyo hapo juu!
Yaani wapewe hongo waipigie ccm!...lakini nasikitika kuwa wanajimaliza, they can take my word to any commercial bank!
 
Acha watumie pesa zao! Wangeziweka kwa ajili ya pension watakapotoka tarehe 31!
 
Mbona sheria ya gharama za uchaguzi inakataza
 
Yaani hadi leo bado hujajua kuwa CCM wameshashinda uchaguzi!?Kinachofanyika tehere 31/10/10 ni kuthibitishwa tuu,poleni chama dume.
 
Waache wawalipie kwenda kupiga kura, halafu hao wanaolipiwa wafanye maamuzi yao. Ila sitashangaa kama watawasafirisha na baadae wasilipwe
 
wanachuo wameisha sema hawadanganyiki, hahaaaah, wapeleke hayo magari ya kuwasafirisha, watawaonesha igizo maridhawa.
 
Hata wafanyeje mwaka hue hawapiti

Si naho chadema nao wasafirishe wanachuo amabao watawapigia kura tuone au waka mwombe Ndesambulo awasafirishie wanavyuo toka makwao kwenda na kurudi?? sijui hivi vyama kama kweli vikwasafirisha hao wana vyuo watupe Budget ya kampeni zao itakuwa kufuru sasa

vijana wachkue usafiri, wale alawansi na wakifika wapige kura kwa kiongozi anayefaa na si chama kinachofaa
 
Hima ccm mfanye hivyo mapema na haraka,ole kwa mwanachuo atakayekubali kugeuzwa toilet paper na hao wasakatonge
 
Nlichobaini hadi sasa ni kwamba wengi hawajui utaratibu wa kupiga kura. POLENI SANA! Mi si mwanachama wa chama chochote, nipo neutral. Habari ndio hii:- Kama wewe ulijiandikisha kupiga kura na upo nje ya kata yako ila jimbo ni lile lile, utaruhusiwa kumpigia kura Mbunge na Rais tu, Diwani hautamchagua, kama upo nje ya jimbo ambalo ulijiandikisha, utaruhusiwa kumchagua Rais tu, Mbunge na Diwani hautaruhusiwa kuwapigia kura. KWA MANTIKI HIYO HAO WANACHUO WATAPIGA KURA YA KUMCHAGUA RAIS HATA KAMA WATAKUWA WAPI, ILI MRADI WAWE NDANI YA TANZANIA, So nyinyi mnaosema kwamba wanachuo hawatapiga kura MNAPOTOKA NA MNAPOTOSHA UMMA WA WATANZANIA.
 
Nadhani kwa sasa hoja si urais tu ubunge na udiwani pia. Kwa mfano chukulia jimbo la Ubungo lilivyo. Kura za wanafunzi zinaweza kubadili maatokeo. Na kwa sasa ubunge kwa vyama vya upinzani ni wa muhimu sana 1. Kuongeza uwakilishi bungeni 2. Kupata ruzuku zaidi kuweza kuimarisha vyama vayo. Kwa udiwani, mambo mengi ya maendeleo yanafanywa katika halmasahuri. Kuimarisha Halmashauri ni moja ya njia za kusukuma maendeleo katika ngazi ya chini
 
CCM wapeni hizo hela haraka,

Kura watampa Dr Slaa na CHADEMA, hawawezi kuwa wajinga kupindukia kiasi cha kuzidiwa na ndugu zangu ambao wana elimu ya primary tu, vijijini sasa wansema mwaka huu ni mabadilko tu,

Naomba masharti maana nina ndugu wengi wanaosoma vyuo mbalimbali;
 
Back
Top Bottom