CCM itakutana na tatizo moja kubwa miaka ijayo ukifika muda ambao huwezi kushinda kwa kuiba kura. Tatizo kubwa watakalo lipata ni kwamba viongozi wengi hawana uvumilivu hata kidogo. Hakuna kiongozi anayejua jela likoje, hakuna kiongozi ambaye anaogopa maisha yake kuwindwa na kutaka kuuliwa au kufikiria hivyo, hakuna kiongozi ambaye anajua anaweza kushinda kura lakini akanyimwa kinyemela, hakuna kiongozi ambaye anaona polisi wako kumzuia yeye na haki zake. Kibaya zaidi wengi wa wateule wanaona kuhudumia wananchi ni kama kuwasaidia na pesa za mali za serikali sio za wananchi bali ni zao.
Hadi Rais imefikia wakati anasahau hili na kusema ndege kanunua yeye binafsi au miradi yote ni pesa za watu binafsi na sio za jamii. CCM ina hali ya umayai umayai bila kujua reality. Mfano waziri alijisahau na kufikiri katibu wa CCM ana nguvu Zanzibar kuliko Malim Seif bila kujua kwamba Mkapa alimpigia magoti miaka ya nyuma na kumeshawahi kutokea mauaji makubwa na wazanzibari kuwa wakimbizi mpaka leo. Zanzibar imeshawahi hata kuwa na ugaidi miaka hiyo na kuisha kwa maridhiano na haujaisha kwa jeshi au polisi.
Seif alivyopewa umakamu si kwamba alipedwa sana ilikuwa kutuliza mambo. Huu umayai umayai na upendeleo utaisha maana iko siku itabidi kushinda kwa kura za ukweli. Mika iyajo hata upigaji kura utakuwa tofauti itazidi kuwa ngumu kuiba kura kwa tecnologia ya vitambulisho, camera kila mahali na teknologia ya vifaa vya kupigia kura. Ikifika wakati wa kupiga kura kwa vifaa vya umeme na kila mtanzania atakuwa na kitambulisho itakuwa ngumu zaidi kuiba. Vilevile vyombo vya ulinzi vinabadilika kutokana na watu wakiona wako upande mbaya wanaweza kabisa kurudi kwa wananchi angalieni huko Sudan jeshi limemgeuka Rais na Misri huko hivyo hivyo.