GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Ni wazi kuwa mpinzani mkuu wa CCM ni CHADEMA! Ndiyo maana hata sisi tusio na vyama vya Kisiasa si shida kutambua kuwa kati ya wanasiasa wanaoipa tabu CCM ni Mbowe na Lissu!
Kwa miaka nenda Rudi, kwa mfano, CCM imekuwa ikimzodoa Mbowe kuwa kakaa muda mrefu madarakani. Lakini kama kukaa madarakani ni issue, kwa nini isiwanange na wanasiasa wengine kama akina John Cheyo na Profesa Lipumba?
Hiyo inatosha kutoa taswira kuwa Mbowe anawanyima usingizi. Vinginevyo, wangempuuzia kama ilivyowapuuzia na akina Lipumba na Cheyo.
Leo hii CCM wanalalamika kuwa Mbowe anatumia chopa na msafara wa magari mengi wakati Lissu akitumia gari moja tu, kwamba inasikitisha na hiyo hali mpaka wakiamua kumchangia. Unajua hiyo nayo inachekesha ee! CCM inamuonea Lissu huruma? Kweli? Ama kweli wanasiasa ni "wanafiki" mno!
Kama ni kweli Mbowe anatumia usafiri bora kuliko makamu wake ni sawa kama ndivyo walivyokubaliana, na hakuna cha ajabu. Hata katika nchi huwezi kulinganisha ukubwa wa msafara wa Rais na viongozi wengine. Mkubwa atabaki kuwa mkubwa tu.
Kama CCM haijui, ni bora kada mwelewe aieleweshe kuwa kumsema Mbowe ni kumwongezea mileage kisiasa.
Mwembe wenye matunda ndiyo hupigwa mawe!