Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Kiongozi Mkuu wa CCM aliwahi kuwaambia wananchi waliokuwa wakilalamikia ukubwa wa tozo ya huduma ya choo kuwa, kama hawataki kulipia hiyo tozo, wabakie na mavi yao.
Waziri wa Serikali ya CCM aliwahi kuwaambia wananchi waliokuwa wakilalamikia ukubwa wa tozo ya huduma za kivuko Kigamboni kuwa, kama hawataki kulipa, waogelee.
Kiongozi Mkuu wa UVCCM aliwahi kuwatamkia wananchi kuwa mara ya kwanza risasi zilishindwa kumwua (TL), akija safari hii tutamwua kwa kumdunga sindano. Ni huyo huyo aliwaambia wananchi wa Arusha kuwa ili kuwathibitishia UVCCM ni wanaume, itabidi wawatie mimba wake zao (yaani wake wa wananchi wa Arusha).
Ni waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Serikali ya CCM aliyethubutu kutoa kauli ya kufuru na kuwakera waumini wa kweli wa dini zote, akamtaja Magufuli kama Mheshimiwa Mungu.
Ni waziri wa mambo ya ndani wa serikali ya CCM, aliyewahi kukufuru na kuwakera wakristo kwa kutamka kuwa Magufuli ni kama Yesu.
Ni mkuu wa mkoa wa serikali ya CCM , aliyewahi kutamka hadharani na kuwakera watu wanaomwabudu Mungu, kuwa eti Mungu anatakiwa kumshukuru Magufuli.
Leo Mdude, aliyekuwa gerezani kwa zaidi ya mwaka mzima kwa kuonewa na utawala dhalimu, asiyejua kiundani Rais wa sasa yupoje, alipopewa nafasi ya kusalimia, akatamka kuwa ataendeleza mapambano, kwa wembe ule ule alioutumia kumnyolea Rais aliyetangulia. Kwangu mimi, hii ilikuwa ni kauli yenye ukakasi, na haikustahili kutamkwa dhidi ya Rais Samia, angalao kwa sasa. Lakini nina imani hata Rais Samia mwenyewe atakuwa amesamehe. Huyu mtu kwanza katekwa, kapigwa mpaka kukaribia kufa, kabambikiwa kesi na Serikali ya CCM, akitoka, kwake inakuwa vigumu kumtenganisha mtu binafsi na serikali dhulumati iliyokuwa imemtesa na kumwonea.
Lakini jambo la msingi la kujiuliza, hata kama Mdude katoa kauli mbaya, CCM ina uhalali wowote wa kukemea? Hivi jambazi ana uhalali wa kumlaani mdokozi? Chama kinachoteka wagombea wa upinzani wakati wa uchaguzi, chama kinachofuta wagombea wa uchaguzi wa vyama vingine, chama kinachoongoza Serikali inayoruhusu uwepo wa makundi ya watu wasiojulikana, makundi yanayofanya kazi ya kuua, kuteka, kupoteza watu na kubambikia watu kesi, kina uhalali wa kukemea kauli ya Mdude, kauli isiyo na athari yoyote kwa uhai wa mtu yeyote?
CCM hamna haki ya kumfundisha mtu yeyote ustaarabu. Ninyi ni sehemu ya uharamia mwingi unaofanyika kwenye nchi hii. Hivi Serikali iliyomwonea na kumbambikia Mdude kesi ya madawa ya kulevya, ilikuwa ya ACT au CCM? Hivi serikali iliyoua watu kule Zanzibar kwaajili ya uchaguzi kule Zanzibar ilikuwa ya DP au CCM? Hivi Serikali iliyokuwa inawapora wananchi pesa kwenye accounts zao, iliyokuwa inawabambikia kesi watu za uhujumu uchumi na itakatoshajo fedha haramu, ilikuwa Serikali ya UMD au ya CCM?
CCM muwe na aibu, ninyi ni wa kufundishwa ustaarabu, siyo wa kumfundisha mtu yeyote ustaarabu. Siasa zenu na uongozi wenu ni primitive.
Tunamwombea Mama Samia, hata kama yupo katikati ya uchafu mwingi wa CCM, hekima imtawale, ausafishe uchafu wote. Hilo linawezekana, akidhamiria, akivaa ujasiri, na Mungu akiwa naye daima.