Pre GE2025 CCM Inatengeneza mazingira ya Sintofahamu/wizi Oktoba 2025, kupitia propaganda ya kukubalika

Pre GE2025 CCM Inatengeneza mazingira ya Sintofahamu/wizi Oktoba 2025, kupitia propaganda ya kukubalika

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

mwanamabadiliko

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2010
Posts
938
Reaction score
1,540
Kinachofanyika kwa sasa ni propaganda inayolenga kuhusisha makundi yote katika jamii ionekane yanamkubali

Samia ili uchaguzi wa Octoba hata yakitokea ya 2020 waseme mgombea alikuwa anakubalika.

Ni dhahiri kuwa Katika sehemu ambayo huwa haipendwi CCM ni vyuo vikuu, sasa hii propaganda inayoendelea sina shaka nayo lakini nadhani lengo za propaganda hizi ambazo zinatumia pesa nyingi ni kutengeneza mazingira ya kuchakachua uchaguzi 2025, nadhani ndio maana Chadema imesema no reform no uchaguzi.

Naamini Mapadri, Wachungaji na Mashekhe watawaambia CCM waweke mazingira fair ya uchaguzi, hii ni nchi ya watanzania wote, na si nchi ya kundi fulani , lazima Watanzania wajue hata wao wana nafasi ya kuongoza nchi, hii nchi c ya CCM.

Haya yote yanatokana na Rushwa na Umasikini ndo mana watu wananunuliwa wakaoneshe kila kundi la jamii linaikubali CCM.

Baada ya wanachuo, sasa watakuja wazee, wamama, wakulima, boda boda , machinga, wote watasema tunaenda na Mama, sasa basi uchaguzi usifanyike apewe nchi mama atawale mpaka atakapochoka.

Mimi Suala hili la Uwizi wa Kura nawaachia Mashekhe, Mapadri na Wachungaji mana naamini hawa ndio watu wa haki
 
Back
Top Bottom