CCM inauawa na usajili wa Hayati Dkt. Magufuli uliofedhesha wana CCM

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
Ukiona chama cha siasa kimeishiwa wajenga hoja kwa muda mfupi lazima ujiulize sababu. CCM imejimaliza kwa sababu zifuatazo;

1. Imejiwekea utaratibu kwamba, Mwenye kusema Ni yule tu mwenye cheo ndani ya chama kwa maana mwenyekiti, makamu, katibu mkuu na mwenezi, mawaziri na manaibu,. Waliobaki awaruhusiwi kusema

2. Wana CCM waliojiona Wana nguvu wanapotumbuliwa au kosa nafasi wanabaki kuwa watazamaji, mfano Bashiru, Polepole, Nape, Muongo, Januaro, Kigwangala nk Hawa uwez wasikia wakijibu hoja maaana wakisema wanaonekana wanaingilia kazi au wanajimwambafai.

3. Polisi imeruhusiwa kuwa wakala wa chama si kwakushughulika na wapinzani tu Bali hata wanaccm na amri inaweza kutoka hata kwa mjumbe wa shina ikanakshiwa na kauli ya maelekezo kutoka juu na ukakamatwa.

4. CCM imeruhusu kukosa wafuasi, kundi kubwa Sasa limezaliwa miaka ya tisini. Limekuwa na vuguvugu ya mabadiliko na limekosa basic needs kutoaka serikalini na hivyo kuvalishwa nafsi ya upinzani. Hakuna mbinu yakushawishi kundi hili.

5. Nchi imegeuka Mali ya familia chache, mfano JK anakula pension, mtoto Mbunge, mke Mbunge je wao tu ndio walioumbwa kuwa wabunge? Na wote wamepita kwa nguvu ya dola. Angalia familia za wastaafu jeshini, Kwenye chama na seniour officers serikalini utabaiini kundi la watawqliwa Ni kubwa na linaumia.

Kufuatili mfumo huu na kukua kwa utandawazi tumewafanya Wana ccm baadhi kuunga mkono harakati za upinzani wakitaka ukombozi. Na ndo maaana kwa zaidi ya mwezi Sasa nchi imetamalaki Ukamataji. Unadani watu watazalisha lini, hao wanaokamatwa ndugu zao ni Askari, walimu, Wat mishi wa sekta mbalimbali, je wanafuraia ndugu zao kuteswa? Hatuwezi kuwa tunasambaza hujuma maofisini na maeneo mbalimbali kwa sababu tu CCM imekosa mvuto? Je viongozi wanaona hii athari au wanadhani wanaokamatwa ni Chadema pekee?
 
Yafaa wayatafakari haya kwa kina, wakiendelea kuzika vichwa vyao mchangani ni wao, kwa uzembe mwisho wataishiwa pumzi mchangani, na wataishia kujizika wenyewe vichwa vyao huku wakiviacha viwiliwili juu ardhini.
 
Ukiona chama kilichokuwa kinaingiza maelfu ya watanzania barabarani kuandamana huku kikiongozwa na aliekuwa katibu mkuu wake kinaanza kususwa na kupelekea chama kununua waandamanaji wasiofika hata 20 huku katibu mkuu na viongozi wengine wakiwa majumban kwao na familia zao, ujue tayar chama hicho kishapoteza ushawishi na sasa kinatafuta njia ya kujijenga kupitia huruma ya wananchi na mada dhoofu kama hii. Bahati nzuri miaka inavyokwenda ndo jinsi watanzania wanavyoendelea kuamka na kukaa mbali na hizi propaganda mfu. Ukifuatilia kwa makini utagundua kuwa waleta mada na wachangiaji wa mada ni wale wale, hakuna mbinu mpya ya kuvuna wanachama na wachangiaji wapya.
 
Wewe nae sio mchambuzi wa mambo. Umayarundika tu unataka wasomaji ndo tuchambue.

Kichwa Cha habari ni tofauti kabisa na uliyoandika.
 
Ukiona chama kilichokuwa kinaingiza maelfu ya watanzania barabarani kuandamana huku kikiongozwa na aliekuwa katibu mkuu wake kinaanza kususwa na kupelekea chama kununua waandamanaji wasiofika hata 20 huku katibu mkuu na viongozi wengine wakiwa majumban kwao na familia zao, ujue tayar chama hicho kishapoteza ushawishi na sasa kinatafuta njia ya kujijenga kupitia huruma ya wananchi na mada dhoofu kama hii. Bahati nzuri miaka inavyokwenda ndo jinsi watanzania wanavyoendelea kuamka na kukaa mbali na hizi propaganda mfu. Ukifuatilia kwa makini utagundua kuwa waleta mada na wachangiaji wa mada ni wale wale, hakuna mbinu mpya ya kuvuna wanachama na wachangiaji wapya.
Sawa kwakuwa wewe ndio watofauti umejitojeza kuwaongezea nguvu Wana kijani bambikizi.
 
Jaribu kukaa chini ufikirie kwa makini haya ninayokwambia.. Kwa dunia ya sasa hakuna chama ambacho kitajijenga au kushinda uchaguzi kwa mada za aina hii. Ikiwa mwenyekiti wa chama kikuu taifa kafungwa na wanachama na viongozi wao mbali mbali hawajaonesha mshikamano wa kweli kumpigania kama alivyopiganiwa Bob wine wa Uganda haulioni tatizo? Badala ya kuja na njia mbadala itakayosaidia chama kurudi katika hadhi yake iliyopotea toka ulipofanyika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 baada ya mwenyekiti kumleta mzee wa vairasi kusambaratisha na kuuwa kabisa matumaini ya chama kushika dola, eti unakuja na utopolo ambao haujengi upinzani wala kuibomoa ccm. Ingia usome humu utakuta kuna wenzako washakuja na propaganda za hovyo zaidi ya hii ya kwako, lkn hazikuleta tija wala faida kwa wapinzani badala yake wapinzani na propaganda zao mfu kama hii waliangukia pua.
 
Yaani MÀTAGA yanavalishwa tisheti za Chadema ,zimeandikwa KATIBA MPYA huku yalisema hayataki Katiba mpya!

Sijui yalivalishwa bila kusoma mwandishi kifuani au hayajui kusoma?

sijui kwanini ccm kila wanachofanya wanakosea[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Acha wafu wazike wafu wenzao.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Jaribu kukaa chini ufikirie kwa makini haya ninayokwambia.. Kwa dunia ya sasa hakuna chama ambacho kitajijenga au kushinda uchaguzi kwa mada za aina hii. Ikiwa mwenyekiti wa chama kikuu taifa kafungwa na wanachama na viongozi wao mbali mbali hawajaonesha mshikamano wa kweli kumpigania kama alivyopiganiwa Bob wine wa Uganda haulioni tatizo? Badala ya kuja na njia mbadala itakayosaidia chama kurudi katika hadhi yake iliyopotea toka ulipofanyika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 baada ya mwenyekiti kumleta mzee wa vairasi kusambaratisha na kuuwa kabisa matumaini ya chama kushika dola, eti unakuja na utopolo ambao haujengi upinzani wala kuibomoa ccm. Ingia usome humu utakuta kuna wenzako washakuja na propaganda za hovyo zaidi ya hii ya kwako, lkn hazikuleta tija wala faida kwa wapinzani badala yake wapinzani na propaganda zao mfu kama hii waliangukia pua.
Ni mawazo tu,kwahiyo pale mtaa wa kijani tuko salama sio ila tunaangamiza kwa majirani kwa gharama zozote,sio.
 
Ukiona chama kilichokuwa kinaingiza maelfu ya watanzania barabarani kuandamana huku kikiongozwa na aliekuwa katibu mkuu wake kinaanza kususwa na kupelekea chama kununua waandamanaji wasiofika hata 20 huku katibu mkuu na viongozi wengine wakiwa majumban kwao na familia zao, ujue tayar chama hicho kishapoteza ushawishi na sasa kinatafuta njia ya kujijenga kupitia huruma ya wananchi na mada dhoofu kama hii. Bahati nzuri miaka inavyokwenda ndo jinsi watanzania wanavyoendelea kuamka na kukaa mbali na hizi propaganda mfu. Ukifuatilia kwa makini utagundua kuwa waleta mada na wachangiaji wa mada ni wale wale, hakuna mbinu mpya ya kuvuna wanachama na wachangiaji wapya.
mtaji wa ccm ni wajinga na wasiojitambua.kibaya zaidi polisi,jeshi na uteuzi unafanya watu waogope upinzani
 
Ukiona chama cha siasa kimeishiwa wajenga hoja kwa muda mfupi lazima ujiulize sababu. CCM imejimaliza kwa sababu zifuatazo;

1. Imejiwekea utaratibu kwamba, Mwenye kusema Ni yule tu mwenye cheo ndani ya chama kwa maana mwenyekiti, makamu, katibu mkuu na mwenezi, mawaziri na manaibu,. Waliobaki awaruhusiwi kusema

2. Wana CCM waliojiona Wana nguvu wanapotumbuliwa au kosa nafasi wanabaki kuwa watazamaji, mfano Bashiru, Polepole, Nape, Muongo, Januaro, Kigwangala nk Hawa uwez wasikia wakijibu hoja maaana wakisema wanaonekana wanaingilia kazi au wanajimwambafai.

3. Polisi imeruhusiwa kuwa wakala wa chama si kwakushughulika na wapinzani tu Bali hata wanaccm na amri inaweza kutoka hata kwa mjumbe wa shina ikanakshiwa na kauli ya maelekezo kutoka juu na ukakamatwa.

4. CCM imeruhusu kukosa wafuasi, kundi kubwa Sasa limezaliwa miaka ya tisini. Limekuwa na vuguvugu ya mabadiliko na limekosa basic needs kutoaka serikalini na hivyo kuvalishwa nafsi ya upinzani. Hakuna mbinu yakushawishi kundi hili.

5. Nchi imegeuka Mali ya familia chache, mfano JK anakula pension, mtoto Mbunge, mke Mbunge je wao tu ndio walioumbwa kuwa wabunge? Na wote wamepita kwa nguvu ya dola. Angalia familia za wastaafu jeshini, Kwenye chama na seniour officers serikalini utabaiini kundi la watawqliwa Ni kubwa na linaumia.

Kufuatili mfumo huu na kukua kwa utandawazi tumewafanya Wana ccm baadhi kuunga mkono harakati za upinzani wakitaka ukombozi. Na ndo maaana kwa zaidi ya mwezi Sasa nchi imetamalaki Ukamataji. Unadani watu watazalisha lini, hao wanaokamatwa ndugu zao ni Askari, walimu, Wat mishi wa sekta mbalimbali, je wanafuraia ndugu zao kuteswa? Hatuwezi kuwa tunasambaza hujuma maofisini na maeneo mbalimbali kwa sababu tu CCM imekosa mvuto? Je viongozi wanaona hii athari au wanadhani wanaokamatwa ni Chadema pekee?
Mpinzani ndio anaweza kwenda CCM. Upinzani hakuendeki kumejaa mjaa tuu . Bora ule usibe kuliko kulala na njaa.
 
Back
Top Bottom