Utawala wa CCM ni aibu kwa Afrika, ni aibu kwa Dunia.
Ulimwengu wa leo ambapo Dunia imestaarabika na kutambua kuwa wewe kuwa kiongozi haimaanishi umekuwa binadamu zaidi, mwerevu zaidi, mwananchi zaidi, mzalendo zaidi au na utu zaidi, bado CCM haijalitambua hilo.
Wakati Dunia ya wastaarabu inatambua kuwa utofauti wa vyama vya siasa ni fikra tofauti zinazotokana na mawazo tofauti na nadharia tofauti ya mbinu katika kuongoza watu, CCM inawaona wenye fikra tofauti ni maadui, hawastahili kuishi, hawastahili heshima wala kusikilizwa.
Enzi za Masiha Kristo, Wayahudi hawakupenda kusikia mahuburi tofauti na imani waliyokuwa nayo. Yesu aliwashinda kwa hekima, hoja, maarifa na utambuzi. Wayahudi, kila siku walitafuta sababu ya kumtia hatiani, na mwishowe walimbambikia kesi kuwa alikuwa amefanya uchochezi wa kuwahasisha watu wasimpe Kaizari kodi. Pilato akakataa kuwa hakuona hatia yoyote ile kwa Masiha Yesu Kristo (ambaye ni mwokozi na Bwana wa Maisha yangu ya leo Duniani na mbinguni).
Wayahudi walipokataliwa kuwa mashtaka yao hayakuwa na nguvu, wakabadilisha hati ya mashtaka kwa kauli, sasa wakasema kuwa wao Wayahudi wanayo sheria, na kwa sheria yao imempasa kufa, kwa sababu amejifanya mwana wa Mungu. Pilato akawaambia mtoeni hapa mkamhukumu kwa hiyo shetia yenu. Na hapo ndipo walipotekeleza uovu wao. Wayahudi walikuwa wajinga na vipofu, walimwua Masiha Kristo, hawakujua kuwa kifo cha Kristo ndiyo ulikuwa mwanzo wa Ukristo ulionea leo Dunia nzima. Kwa kupitia kifo, Mungu akajipatia ushindi wa kuwarejesha waliokuwa wake.
Waliyoyafanya Wayahudi enzi za Yesu, ndivyo wanavyofanya CCM leo dhidi ya yeyote mwenye kunena au kudai kilicho haki lakini wasichokitaka wao CCM. Ni serikali ya CCM iliyobambikia:
1) Tundu Lisu, kesi nyingi za uchochezi
2) Freeman Mbowe, kesi za uchochezi, mauaji ya Akwilina RIP, na sasa ugaidi
3) Msigwa, Sugu, Halima, Kigaiya, na wengine wengi kwa makosa ya uchochezu, mikusanyiko haramu, n.k
4) Ni serikali ya CCM iliwanyang'anya pesa wafanyabiashara wa kubadilisha fedha licha ya kuwa na leseni zote.
5) Ni serikali ya CCM ambayo imekuwa ikiwabambikia watu kodi kama njia ya kuwakomoa kama huwaabudu na kuwasifu.
6) Ni serikali ya CCM inayowabambikia kesi watu za uhujumu uchumi ili kuwanyang'anya pesa walizozichuma kwa jasho na haki yao.
7) Ni ndani ya utawala wa CCM, wakosoaji wa sera na viongozi, wamewahi kuuawa, kutekwa, kuteswa na wengine kuuawa.
8) Ni serikali ya CCM ambayo imekuwa ikiendesha chaguzi za kiinimacho
9) Ni serikali ya CCM ndiyo iliyowahi kuyafungia magazeti mengi eti kwa kutoa habari za uwongo, huku viongozi wa serikali mara nyinhi wakiongea uwongo kuwadanganya wananchi, lakini hawajawahi kuwajibishwa kwa namna yoyote
10) Ni serikali ya CCM, kama ilivyokuwa enzi za Masiha, imembambikizia kesi Mbowe, na kila inapoonekana shitaka la mwanzo halina msingi, kama walivyofanya Wayahudi, humbadilisha mashtaka. Lakini ni aheri enzi za Pilato, mahakama yake ilikuwa na kiwango fulani cha haki. Yeye alitupilia mbali madai dhidi ya masiha kuwa amewachochea watu kutokulipa kodi. Alinawa mikono, akawaambia Wayahudi, mkamhukumu kwa sheria zenu, lakini siyo kwa sheria za ile mahakama yake. Pilato wetu anaona kabisa kuwa hakuna mashtaka, lakini anawaambia Wayahudi, karekebisheni, kaandaeni upya, halafu mniletee.
Laana iwe juu ya wote wanaodhulumu haki za Watanzania. Walaaniwe wao, na vizazi vyao katika makundi au mtu mmoja mmoja. Laana itembee nao mpaka siku watakapopatwa na ufahamu kuwa wao si lolote na si chochote zaidi ya wanadamu, zaidi ya Watanzania wengine.
Shetani siku zote hajawahi kukoma kuishi wala kuacha kutenda kazi, alikuwepo wakati wa enzi za Pontio Pilato, nyakati za Hitler, yupo mpaka leo akitenda kazi, anachofanya ni kubadilisha makao.
Walio na tamaa ya kuwa watakatifu, wito wa kinabii kwenu, jitengeni na yule aliye mwovu aishiye kwa sura za walio miongoni mwenu. Kujishikamanisha na shetani hakuwezi kukutenga na shetani, unakuwa sehemu ya shetani.
Mbowe anateseka, anaonewa, anasumbuliwa, lakini ushindi wake ni mkubwa kuliko hapo mwanzo.
Tafakari matendo yako, umeshikamana na shetani kwa tamaa ya cheo, pesa, umaarufu, Au umeshikamana na Bwana wa haki hata kama unatukanwa, unateswa, unaonewa, au kudhulumiwa? Kwa kutegemea umeshikamana na nani, au una ushindi bandia au una ushindi wa kudumu.