LGE2024 CCM itaanguka vibaya mno kwenye uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa na haitaamini

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Li ngunda ngali

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2023
Posts
707
Reaction score
2,572
Matarajio ya CCM kushinda viti vingi vya wagombea wao katika Uchaguzi ujao wa Serikali Mitaa huenda yasitimie kwa sababu ya figisu za wao kwa wao kwenye uteuzi wao wa ndani hali itakayopelekea visasi ndaniyo.

CCM itarajie kisichotarajika kwenye Uchaguzi huo.
 
Ukiona Hao Uliowataja Wameanguka,, Ujue Hao Wengine Watakuwa Mahututi Kama Si Kufa Kabisa.
 
Unaota wewe, Kwanza picha linaanza wanasema kuna watu zaidi ya milioni 30 wamejiandikisha kupiga kura wakati uhalisia ni kwamba waliojiandikisha hawazidi milioni 8

Kiufupi sijaona haja ya kupiga kura na ni mategemeo yangu Ccm ishajipa ushindi wa asilimia 99.99 %
 
Ni kweli, leo nilikuwa mahali nimesikia wana nzengo wakiwa na malalamiko na wanasema wataipigia upinzani hata waweke Jiwe... wenye chama chukueni hatua kuthibiti migogoro huko
 
Pamoja na figisu zote zilizofanyika wakati wa uandikishaji bado unasema itaanguka vibaya? Ubatili mtupu! Ubatili mtupu!
 
Aisee ni kweli waanze kujiandaa kisaikolojia
 
Wewe tu utashinda kwa sababu umejitambua mapema.
 
Kua na imani potofu na kuamini katika ushirikina ni umaskini mbaya wa kiwango cha juu sana sana aise dah 🤣

ati CCM itafanyaje?🤣
 
Reactions: Tui
Kwani kuna uchaguzi hadi useme ccm itaanguka? Matokeo ya uchaguzi tayari yameshapangwa, siku ya kura ni hadaa tu kwa umma na dunia kuwa kuna uchaguzi.
 
Matarajio ya CCM kushinda ni makubwa kwa sababu wapiga kura wanatambua rekodi yake ya maendeleo na mipango inayolenga kukuza ustawi wa jamii.

Wananchi wanahitaji amani na utulivu, na CCM inatoa suluhisho bora kwa changamoto zinazowakabili.

Kwa hiyo, ushindi ni lazima katika uchaguzi ujao.

Nakuombea uhai ujionee hilo ili Uchaguzi ujao kama utakuwa na akili timamu usije kuandika tena pumba kama hii uliyoandika Leo.
 
Swala la CCM kushinda uchaguzi lipo kikatiba labda kama unaota
 
Ni kweli, leo nilikuwa mahali nimesikia wana nzengo wakiwa na malalamiko na wanasema wataipigia upinzani hata waweke Jiwe... wenye chama chukueni hatua kuthibiti migogoro huko
Nyamazeni bhana! Mnawaamsha wa Nini!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…