Pre GE2025 CCM itabaki milele madarakani sababu inaongoza masikini

Pre GE2025 CCM itabaki milele madarakani sababu inaongoza masikini

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Juice world

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2022
Posts
1,982
Reaction score
2,706
Wakuu kama kichwa cha habari kinavyosema, CCM ITABAKI MILELE madarakani sababu ni moja tu wanaowaongoza ni wananchi masikini sana.

Huwa nashangaa mfano mbunge anakuja watu wanamchekeachekea tu yaani ile ya kujipendekeza kwa tajiri nafikiri mmenipata.

Kuna siku kamapeni ilifanyika mkoa fulani na uhifadhi kwa jina ili uzi usifutwe watu walipewa noti za shilingi elfu kumi zikiwa ndani ya ganda la viberiti na mbunge husika nafikiri wanamjua ilikua mtu anarushiwa kiberiti akifungua ndani kuna noti ya elfu kumi!

Pia soma: Hizi ni sababu tatu kubwa CCM itaongoza milele

Sasa je, hawa wananchi walivyokua na njaa na hawajielewi kama hizo noti ni pesa zao za kodi wakamuona Mungu wao wakampa kura na mpaka leo anaongoza na hajawahi kukanyaga Jimboni tangia mwaka 2020.

Sasa je, jiulize ni mikoa mingapi wanafanya hivi? Sasa hapo kuna kitu ili uweze kuiangusha CCM lazima raia wapambane kutafuta pesa wasiwe masikini njaa.
 
Wakuu kama kichwa Cha habari kinavyosema ccm ITABAKI MILELE madarakani sababu ni Moja tu wanaowaongoza ni wananchi masikini sana huwa nashangaa mfano mbunge anakuja watu wanamchekeachekea tu yaani Ile ya kujipendekeza Kwa tajiri nafikiri mmenipata Kuna siku kamapeni ilifanyika mkoa Fulani nauhifadhi Kwa jina Ili Uzi usifutwe watu walipewa noti za shilingi elfu kumi zikiwa ndani ya ganda la viberiti na mbunge husika nafikiri wanamjua ilikua mtu anarushiwa kiberiti akifungua ndani Kuna noti ya elfu kumi Sasa je Hawa wananchi walivyokua na njaa na hawajielewi kama hizo noti ni pesa zao za Kodi wakamuona mungu wao wakampa kura na mpaka Leo anaongoza na hajawahi kukanyaga Jimboni tangia mwaka 2020 Sasa je jiulize ni mikoa mingapi wanafanya hivi Sasa hapo Kuna kitu Ili uweze kuiangusha ccm lazima raia wapambane kutafuta pesa wasiwe masikini njaa
Kutawala milele haiwezekani, kila chenye mwanzo lazima kitakuwa na mwisho. Hakuna marefu yasiyo na ncha.
Hata Dikteta Mobutu Seseseko aliwatangazia Wananchi wote wa Zaire (Congo DRC) kwamba yeye ndiye Rais wao wa maisha nchini Zaire, lakini leo hii Mobutu Seseseko yuko wapi??? Je, bado anatawala nchini Zaire???
 
Back
Top Bottom