Joseph Ludovick
JF-Expert Member
- Aug 11, 2013
- 364
- 468
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kuaminiwa na watanzania kutokana na historia yake, uwezo wake wa kupatanisha itikadi za kisiasa, uimara wa miundombinu yake ya chama, Uongozi, na udhaifu wa vyama vya upinzani. CCM imefanikiwa kujenga misingi imara ya utawala na imesimamia maslahi ya wananchi huku ikikabiliana na changamoto za kisiasa na kiuchumi.
CCM inatokana na TANU na ASP vilivyoongoza harakati za kupigania uhuru mwaka 1961 na Mapinduzi mwaka 1964. CCM imejijengea taswira ya chama cha kupigania haki na ustawi wa watu. Hii imekijengea kuaminiwa na wananchi kuwa mkombozi wa kisiasa na kiuchumi. CCM imeendelea kuongoza mabadiliko muhimu ya kisiasa na kijamii nchini.
CCM imepatanisha na kusawazisha itikadi mbili zinazokinzana—ujamaa na ubepari. Katika miaka ya awali ya uhuru, chini ya uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere, Tanzania ilifuata sera za ujamaa zilizolenga kujenga usawa wa kijamii na kuondoa unyonyaji. Hata hivyo, sera hizi zilikumbwa na changamoto mbalimbali, hasa za kiuchumi, na kulazimisha serikali kufanya marekebisho. CCM ilifanya mabadiliko ya sera zake kwa kuingiza vipengele vya ubepari, ikiruhusu sekta binafsi kukua na kushamiri, huku ikihifadhi baadhi ya misingi ya ujamaa kama vile utoaji wa huduma za kijamii kwa wote. Hii imeifanya Tanzania kuwa na uchumi mseto unaojumuisha soko huria na huduma za kijamii zinazotolewa na serikali, hivyo kusaidia CCM kuendelea kuwa na mvuto kwa wananchi wa makundi mbalimbali.
CCM imejijengea mtandao wa kisiasa ulioenea nchi nzima, kwa kuwa na matawi katika kila kijiji na mtaa, hali inayokifanya kiwe karibu zaidi na wananchi. Hii imesaidia kuwa na ushawishi mkubwa katika ngazi za chini, jambo linaloongeza imani ya wananchi kwa chama. Hii pia imewezesha CCM kuwa na uwezo mkubwa wa kuendesha kampeni na kufikia maeneo mengi, tofauti na vyama vya upinzani ambavyo mara nyingi vinakabiliwa na changamoto za kifedha na kiutawala na vikiwa vyama vya mijini tu. Aidha, CCM imejenga utamaduni wa kujibu mahitaji ya wananchi kwa haraka kupitia sera zake za maendeleo na utekelezaji wa miradi ya kiuchumi na kijamii. Kila rais aliyepita chini ya CCM ameongeza kasi ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya kitaifa, kama vile ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, na madaraja, upanuzi wa huduma za afya na elimu, na kuhakikisha amani na utulivu unaendelea kudumu nchini.
CCM inabadili viongozi wake wakuu kidemokrasia kupitia mfumo wa chaguzi za ndani ambapo wanachama wote wana fursa ya kushiriki. Kila baada ya miaka mitano, CCM hufanya Mkutano Mkuu wa Taifa ambao unajumuisha wajumbe kutoka sehemu zote za nchi, na hapo huwachagua viongozi wa juu wa chama, akiwemo mwenyekiti na katibu mkuu. Mchakato huu wa wazi na wa kidemokrasia unatoa nafasi kwa viongozi wapya na kuchochea ushindani wa kisiasa ndani ya chama. Kinyume chake, vyama vya upinzani hasa CHADEMA mara nyingi hukabiliwa na migogoro ya ndani na kukosekana kwa uwazi katika mabadiliko ya uongozi na viongozi kujimilikisha vyama, jambo linalodhoofisha demokrasia.
CCM imekuwa na rasilimali nyingi zinazoiwezesha kuendesha shughuli zake za kisiasa kwa ufanisi, huku vyama vya upinzani mara nyingi vikikabiliwa na ukosefu wa rasilimali za kifedha kutokana na ufisadi ndani ya vyama hivyo na miundombinu ya uongozi. CHADEMA inahangaika kuunda uongozi wa Kanda ambao tumeshuhudia magenge ya koo yakitaka kuuana kwa sababu uongozi ndani yake ni jambo la mtu badala ya taasisi. Hii imeathiri uwezo wa vyama hivyo kufikia maeneo mengi na kushindana na CCM. Vilevile vyama vya upinzani Tanzania vimekuwa vikikumbwa na migogoro ya ndani na ukosefu wa umoja.
CCM imeweza kutumia udhaifu huu kujijengea kuaminiwa zaidi na wananchi kwa kuonekana kuwa na umoja na uthabiti katika sera na uongozi wake. Migogoro imeathiri uwezo wa upinzani kuwasilisha ajenda zao kwa ufanisi na kujipambanua kama mbadala wenye nguvu dhidi ya CCM kwani qananchi wengi wqnaviona kuwa vyama vya matusi. CCM imeweza kubadilika kulingana na mahitaji ya kisiasa na kiuchumi ya wakati husika, jambo ambalo limechangia uhai wake wa kisiasa. Mabadiliko haya yamehusisha kurekebisha katiba ya chama na sera za kitaifa ili kuakisi mabadiliko ya kimataifa na mahitaji ya ndani.
Soma Pia:
Katika nyakati za hivi karibuni, CCM imekuwa ikitekeleza ajenda za maendeleo kama vile "Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano" ambao umejikita katika kujenga uchumi wa viwanda na kuendeleza miundombinu. Hii imewavutia wapiga kura wengi ambao wanaona CCM kama chama kinachotoa mwelekeo wa maendeleo ya kiuchumi na ustawi wa kijamii. Kwa mtindo huu, CCM bado ipo sana. Utake ndivyo hivyo, usitake ndivyo hivyo pia.