Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 324
- 649
*UCHAGUZI TUNASHINDA KWA TECHNICALITIES NA KWA KURA.*
Na Elius Ndabila
0768239284.
Wakati mchakato wa uchaguzi ukiwa unaendelea, basi ninataka niwakumbushe mbinu za ushindi kwenye chaguzi zozote za kidemokrasia. Uchaguzi wa kidemokrasia Unaweza kuwa na mbinu nyingi za kushinda hasa sheria zikifuatwa. Mbinu kubwa ni mbinu(technicalities) na kura (vote).
Technicalities hii njia inayoweza kumpatia mtu ushindi hata kabla ya uchaguzi. Ni njia ambayo ipo kwa mjibu wa sheria na kanuni zingine za uchaguzi. Technicalities ni njia ambayo mpinzani hutumia kumuadhibu mpinzani wake hata kabla hajapanda jukwani. Ukisikia mtu kapita bila kupingwa wakati waliochukua fomu ilikuwa zaidi ya mtu mmoja basi tambua jamaa kashinda kwa technicalities. Moja ya makosa makubwa yanayowafanya watu kuondoka kwenye mchakato na mpinzani kupita bila kupingwa ni udanganyifu katika ujazwaji wa fomu au makosa mengine yanayoambatana na sheria za uchaguzi ambapo kimsingi mtu fulani anakuwa hakidhi vigezo. Hii ni mbinu ambayo CCM inatumia sana kuwaadhibu wapinzani. Kwenye uchaguzi hata jina lako ukikosea neno moja, hilo hilo linakuondoa kwa kuwa mtu atakuwekea pingamizi.
Ushindi wa pili huu unatokana na VOTE/ KURA. Demokrasia inaruhusu mtu anayepata kura nyingi ndiye atangazwe kuwa mshindi. Na ushindi wa kura huu unaambatana na mambo mengi lakini kubwa watu wanachagua mtu mwenye sera nzuri. Hii ya kura inawaruhusu watu kupambana kwa mda fulani na hatimaye watu kuamua kumpigia mtu wanayemtaka kura nyingi.
Kwa msingi huo unapoingia kwenye uchaguzi lazima kwanza utambue udhaifu wa mwenzako. Udhaifu huo tunaanza kuutafta siku tu anaporudisha fomu. Hapo lazima uipitie fomu yake ili uweze kumuwekea pingamizi na hatimaye kupigwa nje. Ukishindwa kupata weakness yake hapo basi lazima ujiandae kwenda kukabiliana nao jukwaani.
Msingi wa hoja yangu ni kuwa hadi sasa tumesikia maeneo kadhaa CCM imepita bila kupingwa. Hapa CCM wamewaadhibu wapinzani kwa Technicalities. Tiyari CCM wanaingia kwenye uchaguzi wa OCTOBER 28 wakiwa na akiba ya Wabunge na Madiwani.