CCM: Je, bado ni chama cha wakulima na wafanyakazi?

Kwa wanaojua kiswahili...nini maana ya "tyranny"?

Nje ya kiboksi inaendelea...

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=osFKsmjwe6g&NR=1[/ame]
 
Naona unaifanyia CPR maiti! Rev. Kwa imani yangu CCM wote ni mafisadi, sikujua kama na wewe ni mmoja wao!

CCM as revolution party has been dead long a go, doctor Kishoka anaifanyia CPR leo!

I am sick, habari ndio hiyo!
 

Baada ya Kikwete kutangaza ahadi lukuki kwa walimu na wafanyakazi wengine juzi ili azoe kura zao, sasa CCM imeruhusu wakulima wauze chakula nje ili kuwahonga wawapigie kura Oktoba 31. Wamezuia uuzaji wa nje wa mahindi siku zote, uchaguzi unakaribia wanafanya danganya toto halafu uchaguzi ukipita wakirudi madarakani wanazuia tena. Uhuni mtupu huu


 
Iko siku itabidi tukae chini na kuangakia hii evolution ya 1% ya wana CCM ambao ndio wenye kukishikilia chama na kukiongoza jinsi walivyo a nguvu zaidi ya wale 99% walio waaminifu na kuamini kuwa Chama cha bado ni kile kilichomkomba Mtanzania na si kubaini kuwa wao ni wafu na watumwa wa hawa majahili wanaokiongoza.
 

Rev umechelewa sana. Watoto wa mjini wanasema unakumbuka shuka kumekucha? CCM ndiyo hivyo ilishatekwa na mafisadi wataiachia, kama kuna wana wema wa ccm ondokeni undeni chama chenu ama jiungeni na Chadema kwa ajili ya ukombozi wa nchi yetu.
 

Na ni kweli kuwa; Kutokana na uozo uliokikuta chama ... na ufisadi wanyonyaji..( Human Parasites)... wanaokitafuna kwa kasi ya ajabu... Ombwe kubwa la uongozi lilitokea na nchi nzima ikajisikia kusalitiwa na kuwa kama ya tima. Ni Kwa mstakabali huu; vyama vya kirai na dini zote vilipoanza kuingilia na kutaka kuikomboa nchi. Hii ikaazisha mijadala na sana sana ... NYARAKA mbalimbali za Kikristu na kiislam ...kujaribu kujaza nafasi ambayo ingetakiwa kufanyawa na CCM. ...Ni Unyoge na Uzembe wa viogozi wa juu wa ccm uliopelekea kushamiri na kukomaa kwa NYARAKA ZA KIDINI ambazo sasa ... zinapelekea mgawanyiko wa Taifa Kidini na kikabila. MAFISADI WA CCM LAZIMA WATWEKE ZIGO HILO!

Kama CCM ingewachulia hatua sahihi za kisheria Mafisadi 10 waliotajwa na Dr Slaa Mwemba yanga leo hii ..umoja wa Kitaifa ungekuwa juuuuu kiasi ambacho Nyaraka za Kidini zisingekuwa na nguvu yoyoye ya kutishia mgawanyiko wa Kitaifa kwa udini ukabila nk...
 
GreatThinkers,

Naleta kwenu kauli iliyonigusa sana jana ktk kipindi cha JE TUTAFIKA, Dk. Azavel Lwaitama (UDSM) alikuwa mgeni pia, tujadili hasa mwanzo wa TANU na CCM, walengwa wa chama walikuwa kina nani na sasa chama kina milikiwa na kina nani.
"CCM ilianzishwa na vuguvugu la wafanyakazi na wakulima lakini baada ya waasisi na waanzilishi wa chama hiki kuitwa mbele ya haki, wamebaki mamluki. Matokeo yake chama hiki kimekuwa si cha wale walengwa, mafisadi wameingia sasaivi wakulima na wafanyakazi hawana nafasi tena"

Alisema mwanachama huyo Mfu wa CCM,
maana hata yeye kama mfanyakazi ameachwa solemba,
Chama kina wenyewe ndiyo kauli zilizotawala miaka mwishoni mwa TISINI.

Hata kauli ya Marehemu KOLIMBA na baadaye neno kukolimba likaibuka?
alisema "CCM imekosa mwelekeo" nadhani alimaanisha kama kauli ya Dk. Lwaitama

Karibuni.
 
Chama hiki sasaivi wamejaa wezi,

Upuuuzi ulianza mwaka miezi michache tu baada ya Baba wa taifa Kufariki,

Solution ni kuelimisha watunzania ili wajue kuwa chama kimeuzwa kwa mafisadi,

Dawa ni kubadili katiba ili mamalaka yao cheo cha mtalii yapungue,

Tuenende vijijini na kila pahali kuwataarifu wananchi kuwa ile alama na Jembe na Nyundo inamaanisha kumtandika mwananchi nyundo kisha jembe linatumika kumfukia.
:whoo:
 
Ccm ni ya matajiri siku hizi ndo mana anayetoa kikubwa ndo anathaminika
 
Mimi nimeshasema na nitasema Tena.

Hata wajenge barabara ya juu kuunganisha Mlima Kilimanjaro na Meru hawapati kura yangu milele

Si si Em ya sasa haijui kabisa kama kuna mhujumu uchumi.

Mtu kwa upuuuuzi wake anatuingiza ktk madeni yanayotugharimu kizazi kizima.

Yaani Unazaliwa na Deni ambalo ailiyesababisha anatanua Boston?
 
Chama Cha Mapinduzi – CCM ambao kwa sasa wanajulikana wakati mwingine kama ‘wanamagamba’ katika falsafa yao mpya ya kujivua magamba eti ili kukirejesha chama katika msingi wake wa awali wa kuwatetea wanyonge yaani wakulima na wafanyakazi ni usanii mtupu.

CCM ya Mwl. Nyerere ilikuwa chama kilichoshika hatamu. Kupitia sera ya ujamaa na kujitegemea chini ya Azimio la Arusha njia kuu za uchumi zilimilikiwa na wananchi wakisimamiwa na chama kupitia serikali. Viwanda vilijengwa na kumilikiwa na wananchi; makampuni, mashirika makubwa yalikuwa ya umma.
Aidha, wakulima walikuwa chini ya vyama vya ushirika ambako waliuza mazao yao na kupata pembejeo. Wafanyakazi walikuwa na moyo kwa kazi zao. Kila mahali pa kazi palikuwa na tawi la Jumuiya ya Wafanyakazi ambao walitetea maslahi ya wafanyakazi na wakati huo huo menejimenti zilikaa na wawakilishi wa wafanyakazi kujadili mustakabali wa taasisi walizoziongoza. Si hivyo tu, pia kulikuwa na mashina ya chama mahali pa kazi. Mambo hayo yalipangwa hivyo ili kuhakikisha kuwa ilani ya chama inasimamiwa na kutekelezwa.

Sera za CCM ya leo hazijulikani. Haijawa bayana CCM wanasimamia itikadi gani. Chama hiki kimetekwa na wafanyabiashara. Wameingiza biashara ndani ya chama hadi katika serikali yake. Leo hii hakuna mwanachama uchwara (masikini) mwenye uwezo wa kugombea nafasi yoyote ya uwakilishi kupitia CCM. Chama kimewageuza viongozi wake wote kuwa mafisadi (wahujumu uchumi).

Chama leo hii ndicho kinachojenga kwa bidii matabaka katika jamii baina ya walionacho na wasionacho. Bunge ambalo lina idadi kubwa ya wabunge wa CCM wakirubuniwa na serikali yao wamejipitishia mishahara mikubwa ya kutisha, posho na marupurupu kibao ambayo yamewawezesha wabunge hao kuingia katika kundi la wachache wenye nacho. Mathalan, mbunge hadi anamaliza kipindi cha miaka mitano anakuwa amejikwapulia takribani shilingi 12,000.000/- x 12 x 5 = 720,000,000/- + pensheni 45,000,000 jumla 765,000,000/-. Jumlisha mkopo wa gari milioni 90 ambao hulipa nusu yake tu; na mkopo mwingine wa milioni 200. Katika mapato hayo, posho mbali mbali hazijaingizwa, ambazo ni kama milioni 150 kwa mwaka.

Katika mazingira kama hayo huwezi kusema CCM ni chama cha kutetea wanyonge ambao chama hicho hicho kimeridhia wajengewe shule, hospitali na miundo mbinu ambayo iko chini ya viwango kupitia wakandalasi wengi ambao ni madiwani wake. Mazao yao huuzwa bei ndogo isiyolingana na gharama za pembejeo wanazotumia. Wafugaji huswagwa na mifugo yao kupisha wawekezaji na waporaji wa aridhi yao kama huko Loliondo, Ngara na kwingineko. Wachimbaji wadogo wadogo huvurushwa toka maeneo ya uchimbaji, na wakati mwingine huuawa kama huko Nyamongo – Tarime, Bulyanhulu, Geita, Mererani na sehemu nyinginezo kadhaa.

Mpendwa baba yetu wa taifa mwl. Nyerere aliacha viwanda vikubwa takribani 11 ambavyo CCM isiyo ya Mwl. Nyerere imeviuza vyote hata vile imara na muhimu kwa kigezo cha ubinafsishaji na uwekezaji. Mwl. Nyerere aliwahisema alipokuwa anawahutubia wafanyakazi siku ya Mei Mosi mwaka 1995 huko Mbeya kwamba CCM kimekuwa cha mazuzu ambao wanamiliki almasi wanabadilishiwa na wajanja vipande vya chupa nao hubaki kukenua meno kama zuzu. CCM kimekuwa dodoki kinafyonza na kunyonya hata usaha. Kimejaza uozo mtupu katika safu yake ya uongozi. Hakuna anayefaa na aliyesafi kwa vigezo vya Mwl. Nyerere. Mwalimu alimkataa J. Kikwete, J. Malecela na E. Lowasa mwaka 1995 katika mchakato wa kupata mgombea urais kupitia CCM.

Binafsi, sikumbuki lini ndugu hao walijisafisha na kuonekana kufaa tena. Ila lililo bayana ni taarifa kwamba J.Kikwete na Lowasa ni wanamtandao waliohakikisha wanaupata urais kwa mmoja wao kwa fedha ndani na nje ya chama.

Aidha, serikali ya CCM imekuwa msiri mno kuhusiana na fedha za EPA na makampuni tata ya Meremeta, Deep Green na Kagoda. Kama kingekuwa chama cha wanyonge au kurudia misingi yake kuwa chama cha wanyonge basi wawe wazi katika maeneo hayo yote ndipo waanze kuvuana magamba.

Serikali ya CCM ambayo inaficha mikataba ya makampuni yachimbayo madinina taarifa za mapato ya madini yetu haiwezi kuwa chama cha wanyonge kamwe. Serikali imeshuhudia wawekezaji sekta ya madini wakiwauwa wananchi wakiwatumia polisi wanaolipwa mishahara yao kupitia kodi za wananchi. Huko Mara wawekezaji wameharibu mazingira kwa kutiririsha maji yenye sumu kwenye vyanzo vya maji watumiayo wananchi na mifugo yao. Mifugo na watu wamedhurika kwa kutumia maji hayo.
Chama hiki hakiwezi kurudi katika misingi yake kwa bajeti tegemezi kila mwaka. Asilimia 70 ya bajeti hutumika kwa matanuzi na maisha ya kifahari ya viongozi kuanzia ngazi za wilaya hadi taifa. Asilimia 30 inayochangiwa na wafadhili katika bajeti ya kila mwaka ndiyo hutumika kwa maendeleo. Wafadhiri wakigoma serikali hukosa mishahara ya watumishi wake na huduma hudhorota. Hospitali hukosa dawa na vifaa muhimu kwa tiba.
Kwa mfumo wa bajeti inayopitishwa na wabunge wa CCM kila mwaka, shule ambazo watoto wa wakulima na wafanyakazi husoma zitakosa walimu bora, vifaa vya kufundishia, majengo na hospitali ambako wanyonge hutibiwa, milele hazitajitosheleza kwa waganga, wauguzi na kukosa vifaa vya tiba.

Kwa Azimio la Arusha ambalo CCM ya baada ya Mwl. Nyerere ililifuta, lilitumika kuondoa matabaka kielimu. Mwalimu alitaifisha shule za madhehebu mbali mbali ya dini ili kuwawezesha watoto wa wakulima na wafanyakazi waweze kusoma pasipo vikwazo vya dini, ukabila na kipato. Yeye mwenyewe mwalimu alisomesha watoto wake katika shule hizi hizi.
CCM ya sasa, haijashika hatamu, ila yenyewe ndiyo iliyoshikwa hatamu zake na mafisadi na mabepari uchwara. Kwa mfumo wake huu haiwezi katu kurudi katika misingi yake. Sekretarieti ya CCM inatumia mbiu hii, “ Nitasema Uongo Daima Ukweli kwangu Mwiko!”. Kwa maana wanajua ukweli wote kwamba CCM hakina ubavu wa kurejelea misingi yake kwani hakina itikadi wala sera inayoeleweka, hakiwezi kutoka hapo kiliponasa kamwe….Sijui.
 
Tokea mwanzo hakikuwa cha wakulima na wafanyakazi !
 
Ahadi za mwana CCM - Je wanaweza kurudi kwenye maadili haya?

1) Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni moja,
2) Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote;
3) Nitajitolea nafsi yangu kuondoa umasikini,ujinga,magonjwa na dhuluma,
4) Rushwa ni adui wa haki.Sitapokea wala kutoa rushwa,
5) Cheo ni dhamana,sitakitumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu,
6) Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote,
7) Nitashirikiana na wenzangu wote kuijenga nchi yetu,na;
8) Nitasema kweli daima,fitina kwangu mwiko.

Kujivuga gamba ni pamoja na kuzirudia hizi ahadi 10 za mwana CCM wa tarehe 5/2/1977
 
Mbona wafanyakazi walisha katazwa mambo ya vyama.
Ndio maana hakuna matawi ya vyama maofisini tena.
Sasa hivi kimebaki kuwa chama cha mafi--Gamba kutoka taabu
 
Inawezekana tu kama kutafanyika mapinduzi makubwa ya namna ya kupata viongozi tofauti na ilivyo sasa ambapo wanapatikana kwa kujuana kindugu, kirafiki, kiushirika wa kifisadi, kwa kujikomba n.k.
 
Kwahiyo hawasemi kidumu chama cha Mapinduzi?
Idumu Siasa ya Ujamaa na Kujitemea?
Zidumu Fikra za Mwenyekiti wa CCM (JK)?

Wow Sasa wanadumiza nini Matumbo yao?
 
Je, chama hiki, CCM, bado ni cha wakulima na wafanyakazi? Kinalinda na kutetea maslahi yao? Viongozi wake ni wa tabaka lipi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…