Je, chama hiki, CCM, bado ni cha wakulima na wafanyakazi? Kinalinda na kutetea maslahi yao? Viongozi wake ni wa tabaka lipi?
hapana
Wadau na wanachama hai wa CCM hili swali liliwahi kuzungumziwa kipindi kile cha falsafa ya kujivua Gamba..walizungumzia meengi lakini moja lililonipa moyo lilikuwa ni kurudisha Chama kwa wenye chama yaani Wakulima kule vijijini sio wakulima Mafisadi na wafanyakazi sisi wenye mishahara kiduchu..lakini matokeo yake Chama bado kimetekwa na wafanyabiashsra wakubwa na matapeli wanang'ang'ania vyeo wanatawala Chama.
Jaribu kupitia Wenyeviti wa Chama kwa sasa wa Mikoa mbaka Wilayani wengi ni wenye biashara zao hata viwanda.
Ningependa Chama kirudi kwa Wakulima na Wafanyakazi kwani ndio lengo kuu la chama na madhumuni aliyoyafikiria Mwalimu Nyerere...tunazidi kusibiri huku tulipo!!