Elections 2010 CCM jimbo la Manyoni yatamka; haitawabembeleza wasiotaka kuipigia kura

Elections 2010 CCM jimbo la Manyoni yatamka; haitawabembeleza wasiotaka kuipigia kura

Malafyale

Platinum Member
Joined
Aug 11, 2008
Posts
13,833
Reaction score
11,173
Chanzo cha Habari hii ni Gazeti la Tanzania Daima;13 August 2010

walidai inaonyesha wazi kuwa chama kimekuwa na tabia ya kumbeba Chiligati kwa kuwa anayo nafasi kubwa katika chama hicho jambo ambalo linaondoa demokrasi ya kweli katika siasa za Jimbo la Manyoni Mashariki.


Wakiendelea kutoa maelezo juu ya msimamo wao walidai kuwa kama mgombea huyo ataletwa katika jimbo hilo kura zao watazielekeza katika chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Walisema kwa sasa siasa hazilengi kunufaisha chama bali kinachotakiwa ni kiongozi gani ambaye amesimama kwa niaba ya wananchi kwa malengo ya kuwaletea maendeleo wananchi na si porojo.
Kwa upande wake katibu wa CCM, Wilaya ya manyoni Mathias Shindagashi alipoulizwa juu ya suala, suala hilo alisema kuwa wale wasiotaka kukipigia kura chama hicho waache wala hawabembelezwi
 
Duh, kazi ipo mwaka huu! viongozi wanalopoka lopoka tu!
 
Kauli ingine ya kusikitisha kutolewa dhidi ya watz wasio na hatia.Hawa CCM nahisi wamelewa madaraka kwa msingi wa ukiritimba uliofikia hatua kuhisi kuwa hata kama watz lukuki hawataipigia kura wao watashinda uchaguzi!

Wakati vyama vingine vya siasa vipo tayari kumbembeleza hata mpiga kura mmoja avutiwe na chama husika ili wapate kura hiyo yake moja tu,wao CCM hawajali hata watz maelfu wasipowapa kura zao !

Alianza JK na TUCTA sasa kaingia Katibu wa CCM-Wilayani,inasikitisha kweli jamani;na kwa kauli hii ya hovyo hovyo toka kwa afisa wa ngazi za juu wa CCM-Wilaya bado Chiligati atashinda Ubunge wa Manyoni-Mashariki?
 
Yetu macho mwaka huu!
Kiranja mkuu kaikataa kura za wafanyakazi,monitor naye hazitaki za darasani kwake!Jana Mbeya vijijini wamerudisha kadi za CCM mpaka kieleweke kama mgombea walompigia hatorudishwa kwenye nafasi yake...
mbona rahaaaa!
 
MBONA CCM INAKUFA KIAJABUAJBU NAmNA HII? MPKA TUKIFIKA OCTOBER KUTAKUWA NA CCM KWELI?
 
Back
Top Bottom