Godluck Ole Medeye.
Nikimfahamu Ole Medeye kuanzia miaka 1990s wakati huo akifanyakazi ofisi ya Mkuu wa Mkoa Arusha kama ofisa utawala/utumishi.
Nakumbuka wakati huo Mkuu wa Mkoa alikuwa Col Tarimo na RDD alikuwa Ritahiwa sijui kama jina liko sahihi sana.Ole Medeye alikuwa akisimamia idara ya afya katika masuala yote ya ajira,kupanda cheo na kuhamisha watumishi wa Idara ya Afya.
Ole Medeye aliacha kazi yake rasmi ya kusimamia Idara ya afya na kukimbilia kazi ya usaidizi Mkuu wa Mkoa.Watumishi wa Idara ya Afya walijikuta wakikosa msaada kwasababu Medeye mara nyingi alipenda kazi za kumsaidia Mkuu wa Mkoa kwakuwa zilikuwa na maslahi zaidi hasa safari za Wilaya mbali mbali.Ifahamike wakati huo Mkoa wa Arusha ulikuwa mkubwa kweli kweli kabla Mkoa wa Manyara haujazaliwa.
Katika mambo ambayo ninayakumbuka sana kuhusiana na Medeye ni tabia yake ya kujikweza,kudharau wengine na kupenda sana kuanzisha migogoro.Tabia hii pia ilijitokeza wakati akiwa Mbunge wa Arumeru na Naibu Waziri wa Ardhi.
Kabila la Waarusha walikuwa na utamaduni wa kukutana eneo la Arusha Technical College ambalo ni maalumu kwa ajili ya mila za😵le Medeye akiwa Mbunge aliandaa mkutano kwa lengo la kupambana na Lema Godbless ambaye ni Mchagga kwamba wachagga wamejazana sana Arusha,wamenunua ardhi nyingi na kwamba sasa ni wakati wa waarusha kutawala mji wao.Hii vita inafanana kwa kiasi fulani vita aliyoianzisha Mbunge wa zamani Mzee Solomon Ole Saibul akitaka wachagga na wapare waondoke Arusha jambo ambalo Mwl Nyerere alilikataa kwa hoja nzuri na ndio ukawa Mwisho wa Ole Saibul kisiasa kwani aliyekuwa mshindani wake Marehemu Mzee Mbagga alimwangusha.
Ukifuatilia siasa za Ole Medeye utakuta ni mtu anayependa ukubwa,madaraka na kupata fursa za kiuchumi kupitia madaraka.Baada ya kujiunga CHADEMA alipewa fursa ya kugombea nafasi ya spika wa Bunge la JMT akashindwa kwakuwa wabunge wa CCM ni wengi.Ukinda mbele zaidi alihitaji kuwemo katika nafasi za ujumbe wa Kamati Kuu ya CDM alipoona hakupata nafasi akatimkia chama cha Mzee Mapesa (Cheyo).Akajitolea nyumba yake kwajili ya ofisi a chama na kuanza kujenga mizizi katika mkoa wake wa Arusha.Mzee Cheyo alipogoma kumwachia nafasi ya mwenyekiti akarejea CCM na sasa anataka ubunge na pengine uwaziri.
Ole Medeye ni mtu wa kupenda madaraka,kwasasa anaona fursa ipo CCM.Ni mtakie kila la heri katika safari yake.