the guardian 17
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 395
- 570
Kunazidi kuchangamka
===
Chama Cha Mapinduzi wilaya Ya Kibaha mkoani Pwani kimempa tuzo ya pongezi Mkuu wa wilaya ya Kibaha Mjini, Nickson John Simon Nikki wa pili kwa usimamizi bora wa utekelezaji wa ilani ya CCM wilayani humo.
Wilaya hiyo chini ya uongozi wa DC Nickson Simon makusanyo ya Halmashauri kutoka yamepanda kutoka Bilioni 7 hadi Bilioni 12.
Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo, DC Nikki wa pili amesema "Hii Tuzo imetokana pia na miradi ya ujenzi na umaliziaji vituo vya afya Tangini, Pangani, Kongowe kupitia mapato ya ndani. Pia ujenzi wa shule ya English medium kupitia mapato ya ndani, tumetoa mikopo ya Tshs Bil. 1.2 kwa vikundi kupitia mapato ya ndani"
Soma Pre GE2025 - Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Aida khenani asema fedha za maendeleo zinazotolewa siyo za CCM wala siyo za 'baba zao' ni kodi za wananchi
"Pia tunajenga parking ya kisasa ya malori na kituo cha mafuta kupitia mapato ya ndani, tumepeleka fedha za uboreshaji barabara kila kata kupitia mapato ya ndani na madawati elfu 4 kwa shule za msingi na sekondari kupitia mapato ya ndani. Pia tumekamilisha majengo ya mama na mtoto hospitali ya wilaya kupitia mapato ya ndani na tunajenga jengo la mama na mtoto katika kituo cha Afya Kongowe kupitia mapato ya ndani"-
Source: Clouds Tv