Pre GE2025 CCM Kilimanjaro wamjibu Mbowe na Lema

Pre GE2025 CCM Kilimanjaro wamjibu Mbowe na Lema

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Ndagullachrles

Senior Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
153
Reaction score
161
Chama cha Mapinduzi (CCM)mkoa wa Kilimanjaro, kimejibu mashambulizi yaliyoelekezwa kwa chama hicho na serikali kutoka kwa viongozi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Mwenyekiti Freeman Mbowe na mwenyekiti wa Kanda, Godbles Lema.

Vigogo hao wa chama cha upinzani walifanya mikutano ya hadhara pamoja na maandamano mwezi April na mwanzoni mwa mwezi huu ambako pamoja na mambo mengine walikosoa vikali serikali ya chama cha mapinduzi chini ya jemedali Daktari Samia Suhulu Hassan.

Leo Chama cha Mapinduzi mkoani Kilimanjaro kimekutana na wanahabari kutoka vyombo mbali mbali na kujibu mapigo kwa kutoa Taarifa ya miradi iliyotelekezwa katika kipindi cha miaka mitatu ya serikali ya awamu ya sita na pesa zilizopelekwa kwenye mkoa huo kwa kipindi hicho.

Katika mkutano huo na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi mdogo kwenye ofisi kuu ya ccm mkoa,katibu wa Itikadi na uenezi mkoa wa Kilimanjaro ,Abraham Urio ,ametaja mafanikio makubwa yaliyofanywa na serikali Katika kipindi cha miaka mitatu .

Amesema Katika kipindi hicho, mkoa wa Kilimanjaro umepokea jumla ya shilingi Bilioni 828.75 ambako miradi 1,190 ya maendeleo imetekelezwa .

Miradi hiyo ilijikita kwenye nyanja ya Elimu,Afya,Maji,Ujenzi,Uchukuzi na usafrishaji,Nishati,Utalii,Ardhi ,mifugo .

Amesema sehemu ya fedha hizo imezinufaisha Kata wanazotoka Freeman Mbowe na Godbles Lema ambao ni wazaliwa wa mkoa wa Kilimanjaro .

'Na Katika hiyo miradi 1,190 imegonga mpaka kwenye kata aliyozaliwa Mbowe,Kata aliyozaliwa Lema,kote huko maendeleo yamepelekwa na serikali inayoongozwa na Daktari Samia Suhulu Hassan"

Urio aliyekuwa ameongozana na Katibu wa Itikadi na uenezi wilaya ya Mwanga,Rodgers Msangi,amesema ,shilingi Bilioni 97.02 ziliekezwa sekta ya Elimu ambako ilihusisha ukarabati pamoja na ujenzi wa madarasa mapya 1,836.zikiwamo shule za msingi na sekondari 26.

Amesema kiasi hicho cha pesa pia kilihusisha ujenzi wa mabweni 106,ujenzi wa matundu 3005 ya vyoo,ujenzi wa maabara 186 kwenye shule shikizi, vyuo vikuu na vyuo vya kati vinane.

Kuhusu utekelezaji wa miradi ya kuwakwamua wananchi kiuchumi,Katibu huyo wa Itikadi na uenezi amesema mkoa ulipokea shilingi Bilioni 10.9 kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF)na kuzinufaisha kaya maskini 41,709 ikiwa ni mkakati wa serikali kuwawezesha wananchi kiuchumi.

Amesema kati hizo shilingi Bilioni 3.49 zimetoa ajira kwa walengwa ambako miradi 604 imetekelezwa ikiwamo miradi ya kubusti.

"Haya yote ni mafanikio ya utelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya ccm ya 2020-2025".

"Tutaenda kwa wananchi Jimbo kwa Jimbo kuwaeleza mafanikio haya ya miaka mitatu ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Daktari Samia Suluhu Hassan",alihitimisha Urio.
 
Mwanachama wa ccm ana isemea serikali kwani msemaji wa serikali wa huo mkoa yupo wapi?.
 
Back
Top Bottom