Nimekuwa nikisikitishwa sana kwa jinsi chama cha mapinduzi inavyotaka kuharibu mfumo mzima wa mchakato wa katiba mpya. Na kwa jinsi hiyo watanzania tukatae utumwa huo wa fikra unaotaka kuletwa na ccm. Serikali tatu ndio maoni ya watanzania wengi. Lugha ya kusema eti muungano unaweza kuvunjika au gharama ya kuendesha Serikali tatu ni mzigo huo ni uongo mtupu kwani Tz ni nchi Tajiri sana lkn Viongozi na familia zao ndio wanufaika wakubwa wa uchumi wa nchi. Warioba na kamati yake yote ni watu wasomi na wenye uelewa mpana na wamesikiliza maoni ya wananchi na katiba inayotokana na wananchi ndio tunayoitaka. Ccm wapambane na katiba yao ya chama na sio ya Nchi. Hizi kauli za serikali mbili tumechoka nazo na kama Zanzibar inaishi tunataka na Tanganyika iliyozikwa ifufuke. Najisikia fahari sana Tanganyika kufufuka. Amen.