Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
CCM soon inaelekea kutimiza miaka 50. Lakini kuna mambo ndani ya chama hicho bado haya-make sense kabisa.
Kwa hivi karibuni, huko Dodoma kulikuwa na tukio la kumsimika Steven Wasira kama Makamu Mwenyekiti wa chama hicho.
Maana yake ni kwamba, Wasira anakuwa Mwanaume 8 kushika nafasi hiyo ndani ya chama hicho, ambacho kinajinasibu kutoa nafasi sawa kwa wanawake.
Ina maana katika miaka 48 ya tangu kuanzishwa kwa CCM hakuna mwanamke hata mmoja aliyeweza kukidhi vigezo au kuwa na ushawishi wa kuwa Makamu Mwenyekiti?
Kama CCM ina Mwenyekiti Mwanamke, inashindikana nini kuwa na Makamu, Katibu au Mwenezi Mwanamke?
Naomba nisisitize kuwa, huenda baada ya Rais Samia kuondoka kwenye nafasi ya Uenyekiti, wanawake wa CCM wasitegemee kupata nafasi kubwa kubwa ndani ya chama hicho.
This was the only time (kwa kuwa Mwenyekiti ni Mwanamke) ya wanawake wa CCM kuonja kiti cha Umakamu au Katibu Uenezi.
Soma pia: Rais Samia aweka rekodi mbili CCM katika harakati za kuwawezesha Wanawake kisiasa
Mnaweza kusema labda mimi ni mfeminia napendelea wanawake, haya kwenye suala la umri pia tusemeje.
Wasira alikuwa ana miaka 23 alipopata kuwa Mbunge na sasa ana miaka 80. Ni kitu gani ambacho analeta kwenye chama, ambacho hakuwza kuleta kwenye miaka 57 iliyopita
CCM ina Makonda, January Makamba, Nape Nnauye na wanachama wengine wengi ambao wana nguvu na energy ya kudumu kwa muda mrefu zaidi kwenye chama but instead they chose an 80 year old veteran?
Hivi mtu kama Wasira anaweza kushindana na makeke ya mtu kama Tundu Lissu? Ni rahisi zaidi kwa mtu kama Makonda na Ali Hapi kupambana na Lissu au huyo Wasira?
Sijajua ni vigezo gani vimetumika lakini uteuzi wa Wasira ni a slap on the face kwa UWT na UVCCM.