Rais2020
JF-Expert Member
- Jul 14, 2016
- 3,248
- 5,537
Amani itawale wana jf wote.
Imezoeleka kuwa kila baada ya miaka mitano ya awamu ya kwanza kwa kila rais anayeingia madarakani kupitia CCM huwa wanautaratibu wa kumwachia tena amalizie awamu ya Pili ya miaka mitano iliyobaki ili akamilishe miaka 10 ya awamu yake ya uongozi.
Katika kuendelea kukusanya mawazo kutoka kwa wanasiasa nguli wa CCM ili kutaka kujua wanauonaje uongozi wa mhemshimiwa sana.
Katika hali ya kushangaza kabisa mmoja wa kada nguli wa chama hicho akiongea na mimi bila kificho akiwa na wenzake alisema " tunashangaa awamu hii mambo yanaenda hovyo hovyo na hii itatufanya sisi kufanya maamuzi ya ajabu 2020 katika kumpata mgombe wa ndani kukiwakilisha chama".
Wanachama hao na wenye nafasi kubwa kabisa katika baraza la mawaziri walienda mbali zaidi na kusema " inaumiza sana nchi kuendeshwa bila kufuata misingi ya katiba".
Wanachama hao walinipa mawazo mengi na kunitia moyo ili mwaka 2020 niweze kugombea uraisi maana hata wao walisema watamweka mgombea ambaye ni kama akinishinda basi atawaongoza wananchi kwa kufuata katiba ya nchi,atasikikiza vilio vya watumishi Hewa,ataboresha afya na elimu.
Kiukweli wanachama na makada HAWA nguli wa chama pendwa walinitia moyo sana na sasa najipanga kwa ajili ya kuhakikisha nainyakua nchi hii maana yule mheshimiwa mwenye uwezo wa kupiga push ups hatagombea tena.
Aidha niwaombe wananchi na wapiga kura wangu wavumilie hii hali maana miaka minne iliyobaki sio mingi sana na 2020 Wananchi bila kujali kama ni tajiri au masikini wataishi kama malaika na sio kama mashetani.
Mwisho. Nawaomba mjifunge mkanda kuelekea 2020.
Rais2020
Rais wa mioyo ya watu
Nitarejesha matumaini yaliyopotea kwa watanzania.