Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Hivi sasa unapotembea kwenye miji mikubwa hapa nchini utakutana na mabango ya wagombea wa CCM, ambayo yamebandikwa kila mahali, hadi kwenye vichochoro, hadi inatia aibu na kuleta kichefuchefu!
Wakati hayo yanafanyika kwa upande wa CCM, kwa kutapanya ovyo pesa zetu za walipa kodi, hali ni mbaya mno kwa wapinzani ambao hata mikutano yao ya kampeni inasuasua!
Nimekuwa nikijiuliza hivi chama ambacho siku zote kinajinasibu kuwa ni chama cha wanyonge, inakuwaje hivi sasa kitumie mabilioni kwa mabilioni ya pesa zetu walipa kodi wa nchi hii, wakati wafanyakazi wa Umma, hawajaongezewa mishahara yao kwa kipindi chote cha miaka 5 tokea serikali hii ya awamu ya 5 iingie madarakani kwa kisingizio kuwa serikali ni "fukara" haina kitu, kwa hiyo ikawaomba wafanyakazi hao wawe wavumilie tu kwa maumivu hayo wanayoyapatia!
Nimekuwa pia nikijiuliza hivi si ndiyo hawa hawa CCM waliosema kuwa vyama vya upinzani hapa nchini vimekufa na vinasubiri tu vizikwe rasmi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu?
Hivi hawa maccm watawezaje kudai kuwa upinzani hapa nchini umekufa, wakati wameingia mchecheto wa hali ya huu, hadi kusambaza mabango yao uchochoroni?
Wanachofanya hawa maccm ni sawasawa na baba mwenye nyumba analiliwa na mama mwenye nyumba ili amwachie pesa angalau kidogo ya kuwanunulia watoto, angalau "matembele" ili waipitishe siku, baba akitoa jibu kuwa hana pesa, fanya maarifa mengine ili watoto wale........
Hapo hapo mama akimsihuhudia huyo baba anarudi jioni akiwa amelewa chakari!
Katika kutoa kipaumbele cha matumizi, ni lazima nikiri kuwa CCM imebugi step!
Upo msemo wa kiswahili unaosema KIZURI CHAJIUZA na KIBAYA CHAJITEMBEZA.
Hiki wanachokifanya CCM kwenye matangazo ya wagombea wao sina budi kusema kuwa ni sawasawa na kusema kuwa KIBAYA NDCHO KINCHOJITEMBEZA!