Mtyama
Member
- Feb 1, 2008
- 53
- 25
Ndugu wanabodi,
Salaam!
Nianze kwa kusema kwamba, nawapenda sana Wachina na naipenda sana China. Kwa historia, China si tu rafiki zetu; kwa Taifa letu la Tanzania na Bara zima la Afrika, China ni ndugu zetu. Tufikirie pia kama nchi, Tanzania tulivyoipambania China hiyo miaka ya 1970s huko UN hadi China kupata kura ya turufu (veto power) katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC).
Tofauti na nchi nyingi za Magharibi, China huwa haipendelei kushinikiza ushawishi wake kwa nchi rafiki au nchi ndugu kama Tanzania. Vyema tukailewa vyema China, na kama taifa, China ni taifa linalotupenda na kwa hatua kubwa za kimaendeleo China walizofikia, hawapendi kutuacha katika hatua zao hizi za kimaendeleo.
Vyama vingi vya Ukombozi wa Bara letu, vinavyoshindwa chaguzi kuu (karibu vyote), havijawahi kurejea madarakani. Chama chetu tawala, CCM vyema wakatambua kuwa chama cha CPC cha China na kama chama rafiki kwa CCM na kwa vyama vingine rafiki vya Ukombozi vinavyoendelea kuongoza dola, vinasaidiwa kujengewa uwezo wa hata kama vinaposhindwa kwenye chaguzi viweze kuwa na uwezo wa kurejea mamlakani.
Utawala wa Milele
Tanzania kama taifa inaongozwa kwa Katiba, Sheria na Taratibu. Utangulizi (Preamble) wa Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatamka kuhusu Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea na pia kuhusu Siasa za Vyama Vingi. Umilele una Mungu!
Nasema naipenda China kwa sababu China kama ndugu zetu, wanatufahamu fika. Vyema basi nasi tukawafahamu. Rais kutamka kuhusu CCM kutawala milele tena mbele ya delegation ya China inaonekana kuwa kauli ya kimkakati kama vile taifa kuondokana na siasa za kiushindani ila kama tumewaelewa vyema hawa ndugu zetu China, vyema mikakati hiyo kama kweli ndivyo hivyo, basi ikawa kwenye mchakato wa Kikatiba.
China si kwamba hawana Upinzani. Wana vyama 8 vya Upinzani selected kutoka sekta muhimu ambavyo hushiriki kwenye mikutano mikuu ya kitaifa, National People's Congress (NPC) na Chinese People's Political Consultative Conference (CPPCC). Mikakati hii na mingine ya kisekta ndiyo imewafanya China kuwa taifa shindani na lenye nguvu kubwa ya kiuchumi na kiushawishi, duniani.
Mikakati Yetu
Vyema kama taifa tukajitafakari kwa maono (vision), dira na dhima yetu ya wapi kama taifa tunaelekea maana hatujachelewa bado na ndugu zetu China wanatuonyesha njia. Kama China wamekuwa na Baraza Kuu la Kiushauri wa Kisiasa (People's Political Consultative Conference), vyema nasi tukaanza na hawa Viongozi wetu Wastaafu.
Kuwa na Baraza la Kiushauri kwa maoni yangu, kutasaidia kuwa na ushauri mwema na mzuri sana kimkakati hata kuelekea kurasimisha ushauri mzuri na maoni mengine mazuri ya kimaendeleo na kuyaweka katika Katiba yetu.
Hofu kubwa ya CCM ni kushindwa katika Uchaguzi Mkuu, na vyema ikaeleweka pia kuwa kushindwa kwa CCM katika Uchaguzi Mkuu ni elekeo la anguko lake hivyo si rahisi CCM kukubali kushindwa. Pengine ndiyo maana tunawasikia wakuu wa chama wakiyatamka haya, japo binafsi naweza pia kusema kuwa ni katika kupigana 'vijembe'.
Kama 'umilele' unaotamkwa ni katika mipango ya mikakati ya kitaifa, vyema basi CCM kama chama tawala wakaongoza mikakati hii katika sura ya kitaifa ili kupata mustakabali mwema wa kitaifa zaidi na hata baadae nchi kuwa na mikakati endelevu na ya kupiga hatua kubwa za kimaendeleo; kikanda na kimataifa (China Model).
Kusita kuwa na mikakati hii na kwa dalili zinazojitokeza miongoni mwa watu, kuna athari zake, tena kubwa. Binafsi ninaejiita Mpinzani, pia sitoweza sita kupambania haki zetu hizi za Kikatiba na haki zingine za msingi.
Uchumi bora, maisha bora, maendeleo bora; yote haya hayatakuwa na tija kama haki za Kikatiba na zile za msingi kukiukwa (utawala wa milele pasipo haki), sina shaka wengi tutaendelea kupambana katika kujenga Taifa la Haki.
Tusiende ndivyo sivyo hadi hao tunaowaita 'mabeberu' nao kuanza kama vile kutusaidia katika kutafuta hizi haki zinazokiukwa, na hasa wanavyoona tunavyokaribiana zaidi na ndugu zetu, China.
Mungu Ibariki Tanzania
Gerald Josephat Nyerere,
Musoma, Mara.
www.muhunda.com