ndg pepe kale angalia unataka kuzungumza nini hapo....sidhani kama balozi jaka mwambi kawaalika watanzania na marafiki wa tanzania waliopo moscow na vitongoji vyake kuja kushangilia ushindi wa mwenyekiti wa ccm,bali watu hao watakutana hapo kushangilia ushindi wa uchaguzi wa rais,kwa maana hiyo hata ushindi ungeangukia kwa dr.slaa au prof.lipumba bado uhalali wa sherehe hiyo ungekuwepo.pitia tena mualiko wa sherehe hiyo uone maandishi yake...tunawakaribisha kusherehekea ushindi wa rais wa jamhuri ya muungano na kumalizika salama kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.balozi anawawakilisha watanzania wote bila kujali vyama vyao.