Unasikia huyo Kinana, Makamba na Uncle wangu Membe hawapo kwenye system kwa sasa.
Hapa utawakuza kama nini mwishowe watabaki kuwa wa kawaida tu, na wanaweza kutingishwa kama anavyo tingishwa Dos Santos wa Angola na binti yake Isabela.
Akina Besigye walikuwa jeshini tena madaktari binafsi wa Museveni na sasa wanateswa na serikali ya camaraderie(tamka Kamarade kwa kimatumbi ) wao.
Haujiulizi kwanini viongozi kama Kagame, Museveni, Mugabe(R.I.P), Mkuruzinza,na Kabila, kwa nyakati tofauti wameng'ang'ania kubaki madarakani?
Jibu ni kwamba ukiachia tu kile kiti hauna nguvu zozote za kumfikia angalau nusu yule aliyeshika kile kiti.
Kwa hivyo kama akitaka kukukomoa anaweza akakumaliza kishamba tu usibakie hata na senti moja bank karibia zote duniani.
Kibaya zaidi hao akina Kinana hawakufikia ngazi ya majenerali na wametoka miaka mingi huko jeshini.
Haya yote ni kelele za muda tu, na uzuri ni kwamba binadamu wepesi sana kusahau yatapita lakini mwenye nguvu atabaki na donge flani na yeye kama binadamu anaweza kuanza kushughulika na kila mmoja wao.
Usisahu kuwa Lowassa alikuwa mwanajeshi na uliona alipokuwa upinzani kama aliweza kumfanya kitu mwenye majeshi yake kwa sasa.
Mwenye majeshi yake lazima ametengeneza utitiri wa wanajeshi wa ngazi za juu wenye utiifu usio kuwa na shaka kwake.
Membe anajua yeye sio jasusi wa kwanza ambae imewezekana kuwa clipped his wings. Pengine wewe haujui lakini najua lazima Membe anajua.
Na mimi sijaona au kusikia kosa la Membe kwenye zile sauti. Labda kama kuna mambo mengine ya siri mabaya anafanya ambayo haya kuwekwa hadharani.
CCM ya kumtingisha mwenyekiti wake na mkuu wa majeshi imeisha 2015, sasa hivi imerudi CCM ya zamani.
Hata kama mwenyekiti ana hofu juu ya hao wakongwe kuondoka ni suala la kibinadamu tu na ni la muda mwishowe atazoea CCM bila Kinana, Makamba Snr, au hata bila Membe ingawa naona haitakuwa busara kumfukuza chamani Membe.
Wamuache ajitoe mwenyewe kama Lowassa 2015.
Kinana aliomba kuachia nafasi ya ukatibu mkuu,mwanzo akaombwa aendelee, karudia tena kakubaliwa na sasa muda umepita tangu aachie kiti na hakuna jambo lililo kwama, chama hakijakufa.
Sent using
Jamii Forums mobile app