Chama cha Mapinduzi (CCM), kimetoa onyo kwa watu wote wanaojipitisha katika majimbo kutaka ubunge kabla ya muda sahihi, hivyo kitawashughulikia.
Akizungumza katika uzinduzi wa ofisi ya CCM Wilaya ya Newala mkoani Mtwara Machi 1, 2025, Katibu wa Organizesheni wa chama hicho, Issa Ussi Gavu amesema atakayebainika kusumbua ufanyaji kazi wa wabunge na madiwani waliopo madarakani kabla ya muda atashughulikiwa.
"Hatukatazi kuwa na nia ya kugombea ubunge na udiwani, kwa sasa kaa nayo moyoni mpaka muda sahihi utakapofika utachukua fomu na kuomba ridhaa, ila kwa sasa tukikubaini tutakushughulikia," amesema Gavu.
Gavu ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM, amesema nafasi ambazo zimeshajazwa ni ya mgombea urais Tanzania bara na Zanzibar, nyingine zote zipo wazi.
Gwajima na diwani wake URIO wa kata ya KUNDUCHI leo wanafanya BONANZA UWANJA MECCO KUNDUCHI.
Mbunge gwajima alianzishindano ya REDE jimboni kwake maka 2 iliyopita.
RUSHWA NI SEHEMU YA UHAI WA CCM, MKAPA ALIITA (TAKRIMA)