Pre GE2025 CCM kuweni na huruma na wananchi wagombea wenu hawatoshi kupeperusha bendera ya chama

Pre GE2025 CCM kuweni na huruma na wananchi wagombea wenu hawatoshi kupeperusha bendera ya chama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

RWANDES

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2019
Posts
1,788
Reaction score
4,401
Utawala wa CCM kwa sasa umekuwa mgumu kwa nchi wagombea waliopo wote mnawajuwa mmoja ana uraisi wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wote mmeona aliyoyafanya katika kipindi chake na kinachoendelea watu wamepotea hovyohovyo tena bila kificho watu wamepaza sauti hamna kilichofanyika wameamua kumwachia Mungu

Ukija kwenye miradi ya maendelea mwendazake aliacha SGR inaelekea kukamilika kutoka Daresalaam hadi Dodoma , vipande alivyoanzisha kwa kukopa pesa nje kutoka Dodoma hadi Mwanza hadi sasa yamejengwa madaraja tu na wakandarasi wametimuka kwa kukosa pesa,

Wote mmeona ya Dp world viongozi wa dini na wanasiasa wasingepaza sauti hata marekebisho madogo ya mkataba huo yasingefanyika, mimi najiuliza hivi tanzania ya leo niyakukopa pesa ya kutengeneza vyoo vya madarasa?

Mradi wa umeme wa Mwalimu Julius Nyerere unahitaji mashine zaidi ya kumi lakin hadi sasa unamashine tisa tu na bado umeme bei yake haishikiki sasa hapo Mtanzania ana nafuu ipi angali tuliaminishwa bei itashuka ya umeme,watanzania tupime mgombea kwa kucheki mambo aliyoyafanya ndiyo tumpe nchi

Uchawa unaliangamiza taifa, mimi kiujumla ukiniambia huyo mama alichofanya nitakwambia alikopa trion 1.3 za uviko na kila shule za sekondari Tanzania nzima akajenga chumba kimoja cha darasa,kuhusu vituo vya afya mwendazake ameacha amejenga vituo zaidi ya 361 sasa mama yenu amefanya nini wekeni miradi hata aliobuni kuianzisha nakuimaliza .

Mwingine ni mgombea mwenza hakuna ubishi kuwa nikiongozi anayeamini kundi fulani ndiyo linafaa kuongoza nchi haya tumeyaona baada ya kukatwa jina rafiki yake Lowasa na siyo hiyo tu akiwa waziri wa nambo ya ndani mliona wenyewe madudu yaliyofanyika ndani ya jeshi la polisi hadi kupelekea kujiuzulu kwake!

Nachojiuliza hawa watu wamepimwa kwa sifa gani za kuongoza nchi? Au watanzania tumekubali kuburuzwa na kundi dogo ndani ya nchi.
 
Back
Top Bottom