CCM kwa haya yanayoendelea ni kama wanajipaka kinyesi

CCM kwa haya yanayoendelea ni kama wanajipaka kinyesi

Subira the princess

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2018
Posts
3,474
Reaction score
3,744
Wasalam:

Kwa hali ilivyo, na jinsi nchi inavyoendeshwa kwa matamko na kuvunja Katiba, jumlisha kauli kinzani za wana CCM zinazowagawa watanganyika huko mbele itakuwa kazi ngumu kuwaunganisha, maana watu wamepoteza imani.

Mambo yafuatayo yameligawa taifa:
1. Ugonjwa wa Corona
ccm hawa hawa waliutangazia umma wasikubali chanjo wapige nyungu n.k, leo CCM walewale wanahubiri watu wapigwe chanjo ni salama lakini hapo hapo kuna CCM wanaopinga hadharani chanjo akiwemo Askofu Gwajima, Polepole na Musukuma watanganyika wamwamini nani?

2. Katiba mpya
CCM hawa hawa walikusanya maoni ya Watanganyika na kuandaa rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba wakihubiri Katiba Mpya ni muhimu. Leo hii CCM walewale kwa uroho na uchu wa madaraka wanahubiri Katiba Mpya si muhimu bali hii ya chama kimoja ndio Katiba sahihi kwa wakati tulinao. Hapa watanganyika na uzuzu walionao wanawazoom na ipo siku mtakosa hoja kwao, CCM kumbukeni wahenga na mababu zetu walisema, ukiwa mwongo mwongo usiwe msahaulifu.
 
CCM wanachemsha
Katiba mpya waliiweka kwenye ilani yao ya uchaguzi ya mwaka 2015, sasa sijui walipokuwa wanafanya hivyo walikuwa hawajui umuhimu wa maji?
 
Subira umetukumbusha mbali sana. CCM ni genge la wahuni.
IMG_20210707_133022_162.JPG
 
Wazanzibari warudi Unguja na Pemba Watanganyika wapate uhuru
 
Back
Top Bottom