Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Kwa KWELI CCM imekuwa ikitutia aibu kila uchao mbele ya wageni kutoka nje ya taifa letu na wahisani wetu.
NI aibu sana kwa nchi fukara kama hii, chama tawala kwenda kununua mabasi ya kifahari kwa ajili ya kampeni, wakati wananchi wenu wanafukuzwa Hospitali kwa kukosa gloves za kujifungulia.
NI ukosefu wa uzalendo na matumizi mabaya ya rasilimali FEDHA za walipa kodi kuona utitiri wa misafara ya magari ya Viongozi, wakati hata kwa hao wanaotuhisani Hawana utitiri huo.
IGP wa Polisi ana msafara wa zaidi ya Gari tatu.
Mkuu wa majeshi CDF ana msururu mrefu mno.
Spika wa bunge naye ana msafara wake mrefu.
Nabii waziri mkuu naye ana msafara mrefu.
Haya ni matumizi mabaya ya rasilimali.
Uingereza tumeona mara nyingi msafara wa waziri mkuu ni Gari tatu mpaka nne tu.
Leo Tanzania chini ya CCM msafara wa rais una Gari zaidi ya hamsini.
Hivi hawa wanaotuhisani wanatuonaje? Wanatufikiriaje lakini? Je wanatuona tuna fikra sahihi?
CCM ya leo haitaki tena kusikia sera za kujitegemea. Mama anaamini kwamba nchi itaendeshwa kwa yeye kusafiri sana nje.
Sasa wahisani wameanza kukata misaada, je tumejipangaje kama taifa chini ya utawala wa CCM?
Viongozi wa serikali hii ya CCM wapunguze matumizi yasiyo ya lazima, ni aibu sana kwa wabunge kufanya mashindano ya kula.
Nini faida ya shindano kama hili? Huku ni kutukanisha Watanzania.