Elections 2010 CCM labda ingemsimamisha Magufuli

Domhome

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2010
Posts
3,198
Reaction score
3,950
Kwa jinsi hali ya kisiasa na joto la uchaguzi lilivyopanda, binafsi sichelei kuyamka kuwa hakuna kizuizi kitakachomzuia Dr. Slaa kuingia Ikulu baada ya Oktoba 31. Mtu pekee ndani ya CCM ambaye angethubutu kuleta upinzani na kumpunguzia kura Slaa, ni Mh. JPM

Je, unadhani kuna mwingine yeyote ndani ya CCM zaidi ya JPM? endeleza hapa:
  1. JPM
  2. .............
 
JPM= tone la maji safi ndani ya bahari ya maji taka. Hawezi kufanya chochote kwa mfumo wa kifisadi uliomo ndani ya ccm. Wito: it is high time for JPM to join Dr. Slaa
 
JPM= tone la maji safi ndani ya bahari ya maji taka. Hawezi kufanya chochote kwa mfumo wa kifisadi uliomo ndani ya ccm. Wito: it high time for JPM to join Dr. Slaa

Jibaba point mkuu.
Kwa mfumo upi wa chama. Kwa mfumo wa ccm ni vigumu kwake kufanya kazi.
Bingu wa Mutharika aliamua kiume,JPM unadhani anaweza kufanya kama Mutharika?
 
Expected President Dr. Slaa ampe U-PM John Pombe Magufuli; hii ijulikane mapema kabisa na sababu iwe ni rekodi yake safi tangu aingie bungeni
 
..Magufuli ameshachafuka.

..mmesahau kuwa alihusika na zoezi la kuuza nyumba za serikali? tena ana tuhuma za kuwauzia ndugu zake baadhi ya nyumba za serikali.

..pia ana kashfa ya kupendelea jimbo lake la uchaguzi kwa mradi wa ujenzi wa barabara.

..zaidi alitumia ubabe kuvunja kituo cha mafuta kule Mwanza. shauri hilo lilipelekwa mahakamani na ikaamuliwa kwamba serikali[mimi na wewe] imlipe mwenye kituo cha mafuta shilingi billioni 15 kutokana na uzembe wa John Pombe Magufuli.

NB:

..kabla ya kugombea Uraisi, Magufuli anapaswa kuwaomba radhi wa-Tanzania kwa kushiriki maamuzi ya kuuza nyumba za serikali. pia itakuwa vizuri akijisafisha kwa kurudisha nyumba aliyojiuzia na zile alizowauzia ndugu zake.
 
Kwa jinsi hali ya kisiasa na joto la uchaguzi lilivyopanda, binafsi sichelei kuyamka kuwa hakuna kizuizi kitakachomzuia Dr. Slaa kuingia Ikulu baada ya Oktoba 31. Mtu pekee ndani ya CCM ambaye angethubutu kuleta upinzani na kumpunguzia kura Slaa, ni Mh. JPM

Je, unadhani kuna mwingine yeyote ndani ya CCM zaidi ya JPM? endeleza hapa:
  1. JPM
  2. .............

Timu ziko uwanjani kuwajadili wachezaji ambao hawako kwenye vikosi vilivyochaguliwa na makocha wakishirikiana na kamati za ufundi ni kupoteza muda. What do you say?
 
Hizi hoja zote ni nguvu ya soda. CCM itashinda tu uchaguzi na hakuna mwenye akili timamu eti awe tayari kukihama chama chenye maziwa na asali eti ahamie upinzani. muulize vizuri mrema au mpendazoe ili waseme.:amen:
 
..Magufuli ameshachafuka.

..mmesahau kuwa alihusika na zoezi la kuuza nyumba za serikali? tena ana tuhuma za kuwauzia ndugu zake baadhi ya nyumba za serikali.

..pia ana kashfa ya kupendelea jimbo lake la uchaguzi kwa mradi wa ujenzi wa barabara.

..zaidi alitumia ubabe kuvunja kituo cha mafuta kule Mwanza. shauri hilo lilipelekwa mahakamani na ikaamuliwa kwamba serikali[mimi na wewe] imlipe mwenye kituo cha mafuta shilingi billioni 15 kutokana na uzembe wa John Pombe Magufuli.

NB:

..kabla ya kugombea Uraisi, Magufuli anapaswa kuwaomba radhi wa-Tanzania kwa kushiriki maamuzi ya kuuza nyumba za serikali. pia itakuwa vizuri akijisafisha kwa kurudisha nyumba aliyojiuzia na zile alizowauzia ndugu zake.
amejiuzia na hakukwapua sio na alipovunja kituo cha mafuta Mwanza si alitumia sheria husika! na can you substantiate kujenga kwake barara kwao kwa kutumia Cost Benefit Analysis?
 
Well, hueanda na wishiful thinking.. but Slaa akiwa magogoni, halafu akamchukua JPM akwa PM, kwa myaka mitatu, Tanzania itakuwa mbali sana!
 
amejiuzia na hakukwapua sio na alipovunja kituo cha mafuta Mwanza si alitumia sheria husika! na can you substantiate kujenga kwake barara kwao kwa kutumia Cost Benefit Analysis?

Ni kweli mkuu. Na issue ya kujenga barabra kwao sioni tatizo maana yeye ni mbunge anayewajibika kwa watu waliomchagua. Wako wabunge wengi tu ambao walipata kuwa na nyadhifa za uwaziri waliopeleka maendeleo katika majimbo yao mfano Mramba, Msuya etc
 
Hizi hoja zote ni nguvu ya soda. CCM itashinda tu uchaguzi na hakuna mwenye akili timamu eti awe tayari kukihama chama chenye maziwa na asali eti ahamie upinzani. muulize vizuri mrema au mpendazoe ili waseme.:amen:

Enyi Wagalatia msio na akili ni nani aliyewaroga hata muamini kuwa CCM haiwezi kushindwa?
 
Geza Ulole said:
amejiuzia na hakukwapua sio na alipovunja kituo cha mafuta Mwanza si alitumia sheria husika! na can you substantiate kujenga kwake barara kwao kwa kutumia Cost Benefit Analysis?

Geza Ulole,

..Magufuli ameshiriki ktk uamuzi ambao ni hujuma ya waziwazi na hasara kwa taifa hili. halafu Magufuli alikuwa hana aibu kuwabeza wale wote waliojaribu kumtahadharisha kwamba uamuzi wake ni biashara kichaa na utalitia taifa hasara. kubwa zaidi akaanza kuingilia uuzwaji/ugawaji wa nyumba zile na kuanza kuwapa watu wake wasiostahili, kuna tuhuma za undugu-nization.

..kuhusu uvunjwaji wa kituo cha mafuta Mwanza ni kweli Magufuli alitumia madaraka yake kama waziri wa miundombinu. tatizo ni kwamba alishauriwa na wataalamu wake kwamba uamuzi wake ulikuwa unakiuka sheria lakini Magufuli akawa na kiburi. well, shauri liliishia mahakamani na ikaamuliwa kwamba Magufuli alikuwa na makosa na ikaamuliwa serikali[walipa kodi] wamlipe mwenye kituo cha mafuta shillingi Billioni 14.

rmashauri said:
Ni kweli mkuu. Na issue ya kujenga barabra kwao sioni tatizo maana yeye ni mbunge anayewajibika kwa watu waliomchagua. Wako wabunge wengi tu ambao walipata kuwa na nyadhifa za uwaziri waliopeleka maendeleo katika majimbo yao mfano Mramba, Msuya etc

rmashauri,

..hakuna anayepinga ujenzi wa barabara ktk majimbo ya Msuya,Mramba,au Magufuli.

..tatizo ni kile kitendo cha kutumia madaraka vibaya na "kuruka mstari" ktk kupeleka miradi ya maendeleo majimboni kwao.

..that is a very bad company which Magufuli has now joined.

NB:

..kabla ya kugombea Uraisi, Magufuli anapaswa kuwaomba radhi wa-Tanzania kwa kushiriki maamuzi ya kuuza nyumba za serikali. pia itakuwa vizuri akijisafisha kwa kurudisha nyumba aliyojiuzia na zile alizowauzia ndugu zake.
 
NB:

..kabla ya kugombea Uraisi, Magufuli anapaswa kuwaomba radhi wa-Tanzania kwa kushiriki maamuzi ya kuuza nyumba za serikali. pia itakuwa vizuri akijisafisha kwa kurudisha nyumba aliyojiuzia na zile alizowauzia ndugu zake.

Eti mimi huwa naona hakustaili hata kujiuzia hizo nyumba bali alistaili kupewa bure kama shukrani ya kazi nzito ya uwaziri wa Ujenzi uliotukuka. Kwani wewe Joka Kuu unadhani nani katika CCM anaweza kutoa upinzani wa kweli kwa Dr. Slaa katika CCM? Manake ndio hoja iliyo mbele yetu!
 
download
 
Chadema kweli wamelalia masikio, Nani amkabidhi nchi Mchungaji Slaa? Damm!!!!!
 
Back
Top Bottom