CCM Matatani Lindi na Mtwara: Ni kuhusu Korosho

Mwanaukweli

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2007
Posts
4,786
Reaction score
1,715
Na Kennedy Kisula

TAKRIBANI miaka kumi na miwili sasa imefika hakujapatikana ufumbuzi wa kudumu wa soko la zao la korosho katika mikoa ya Lindi na Mtwara. Mkazi wa Kijiji cha Mnolela wilayani Lindi Vijijini, Esimael Nanjuka ameyasema hayo jana wakati alipokuwa akizungumza na mwandishi wa makala haya, amesema kwamba serikali mbili za Rais mstaafu Benjamin Mkapa na Rais Kikwete wameshindwa kupata ufumbuzi wa kuweza kusaidia wakulima wa zao la korosho na kusababisha
kukata tamaa kuzalisha zao hilo.

Alifafanua Rais Mstaafu Benjamin Mkapa wakati wake alitoa ahadi kwamba viwanda vimebinafsishwa kwa sasa korosho zote zitaweza kubanguliwa hapa hapa nchini. Alisema kwa hiyo wakulima wa zao hilo watakuwa na uwezo wa kupata soko la uhakika na kuweza kupanua mashamba kwa minajili ya kuongeza mapato na kuondokana na umasikini. Nanjuka alisema mpaka sasa hakuna viwanda vinavyofanya kazi ya kubangua zaidi ya kusafirisha zilizokuwa ghafi nje ya nchi. Aliongeza kuwa tatizo lilikuwa korosho ghafi hazina soko la uhakika kama lipo ni moja la kupeleka nchini India, na kama zingebanguliwa masoko yake yapo ndani na nje ya nchi.

Alisema kwa hiyo kipindi chote alichokaa Rais Mkapa alishindwa kabisa kupata ufumbuzi na kurithiwa na Rais Kikwete naye anaeleka kushindwa ila serikali zao zinatumia lugha za kisiasa zaidi. Hivi karibuni alitoa ahadi kuwa korosho zinunuliwe baada ya mamlaka husika kukaa pamoja kama Bodi ya Korosho, taasisi za fedha na wanunuzi. Alisema kwenye utekelezaji wake walikubaliana wakulima walipwe malipo ya awali ya Sh 600 na pili walipwe Sh 600 kwa kila kilo. Alisema kwamba hayo malipo ya awali yenyewe wanakopa vyama vya msingi vya ushirika unakaa muda wa wiki moja, siku tano ndiyo unalipwa. Alisema malipo ya awali wanalipwa kwa mwezi huu wa Desemba na haifahamiki ya pili wataweza kulipwa lini.

Aliongeza kuwa hali ambayo inawatia wasiwasi mkubwa wakulima wa kuweza kufanikiwa na kuweza kupata mahitaji yao. Alitoa mfano mkulima ananunua pembejeo ya salfa mfuko Sh 40,000 kama ana ekari kumi ataweza kutumia Sh 400,000 vibarua wa kumfanyia kazi, bado madawa mengine ya kuzuia magonjwa ya ubwiri unga. Alisema kwamba kwa hiyo malipo yake ya awali itabidi alipe madeni kwanza na ya pili afanyie matumizi yake, na hafahamu itakuwa ni lini na kila kukicha vyakula vinapanda bei. Kwa hali hiyo bado umasikini unazidi kuongezeka siku hadi siku kwani mkulima anakuwa anapambana na changamoto nyingi juu ya kazi yake ya ukulima. Alisema inaamanisha wazi mpaka sasa hakuna serikali inayomjali mkulima zaidi ya kumtungia sera ambazo bado hazijaweza kumkomboa. Naye Katibu na Mwandishi Mkuu wa Chama cha msingi cha mazao cha Ushirika Mnolela wilayani Lindi Vijijini, Hassani Kongwa alisema mpaka sasa umoja huo ulishakusanya tani 700 za korosho.

Alisema kwamba tani hizo zina thamani ya Sh milioni 420 zilishatolewa kwa wakulima kama malipo yao ya awali. Alisema kwamba kweli wakulima wanakaa muda wa siku tano au wiki kutokana mfumo wa taasisi za kifedha benki wanataka kwanza korosho ikusanywe na kupelekwa ghalani tayari kupigwa mnada. Alisema baada ya kufika ghalani inatolewa risiti inayojulisha zimepokelewa kiasi cha tani kutoka chama cha msingi na hiyo risiti itapelekwa benki tayari kwa malipo. Aliongeza zinapopelekwa korosho hizo huko huko maghalani mpaka zipokelewe zinachukua siku tatu mpaka wiki, kwani kunakuwa na foleni katika maghala ya Buko na Mtama wilayani Lindi.

Alifafanua sababu ya pili haiwezekani kukaa na fedha Sh milioni 100 mpaka 200 katika masurufu ya fedha katika Ofisi ya Ushirika, zitaweza kuibwa. Kongwa alisema hali siyo nzuri kwa mkulima ni bora zikusanywe korosho na fedha zikiletwa zitolewe zote kwa pamoja. Hata hivyo alisema kwamba mpaka sasa wanunuzi hawajafika maghalani kununua korosho, kwa hiyo hali inaleta wasi wasi mkubwa kwa wakulima, wilayani humo. Hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete aliwaita wadau wa zao la korosho zikiwemo kampuni mbalimbali, Mamlaka ya Bodi ya Korosho nchini, viongozi wa vyama vikuu vya ushirika wakuu wa wilaya na mikoa ya Pwani, Mtwara, Lindi na Tunduru kutoka Mkoa wa Ruvuma.

Alizitaka mamlaka husika kuhakikisha korosho za wakulima zinanunuliwa na kulipwa haki zao zinazostahili, wilayani Kilwa mkoani Lindi. Alisema kwenye kikao hicho kwamba wakulima wanakabiliwa na changamoto nyingi mno kama ununuzi wa pembejeo kutopata soko la uhakika. Aliongeza kwa kusema kwamba hata bei ya korosho nayo iko chini mno ukilinganisha na gharama zake za uzalishaji.

Rais Kikwete alisema kwamba kwa hiyo hali siyo nzuri kwa hiyo Bodi ya Korosho wakutane na kampuni za ununuzi wa korosho waanze kununua wiki hii. Taarifa kutoka Mamlaka ya bodi ya korosho iliyotolewa kwenye kikao hicho na kuonesha viwanda vinavyobangua na kampuni zinazosafirisha nje ya nchi. Taarifa hiyo iliyosambazwa inaleta uchungu kwa wakulima kutokana na kampuni zinazobangua korosho zipo nne zilizopewa leseni na mamlaka husika, msimu wa mwaka huu. Taarifa hiyo ilieleza kampuni zinazobangua zikiwemo South Jumbo Cashwnuts waliopewa leseni namba 0001 iliyotolewa mwezi Novemba 13, mwaka huu, kutoka mkoani Dar es Salaam.

Kampuni nyingine ni Mohammed Enterprises Tanzania (METL) walipewa leseni namba 0002 mwezi Novemba, mwaka huu na Export Trading Co.Ltd wamepewa leseni namba 0003. Kampuni iliyosalia ni ya Cashwnut Company (2005) Ltd yenye namba za leseni ni 0005 kwa ajili ya kubangua korosho.

Taarifa hiyo ilieleza kwamba kampuni zilizopewa leseni za kununua na kusafirisha korosho nje ya nchi ambazo ni ghafi kwa msimu wa mwaka huu ni 29. Hali hiyo inaonesha wazi kwamba korosho nyingi zinasafirishwa ghafi kuliko kubanguliwa.

Kampuni hizo ni Blue Diamond International Ltd, yenye leseni 0001 iliyotolewa Octoba, mwaka huu, mkoani Mtwara. Gefu Agromat Co.LTD wana leseni yenye nambari 0002, ISCON Commodoties LTD walipewa leseni nambari 0003, NIAGRO Business Co. (T) LTD walipewa leseni ya usafirishaji nambari 0004 SAKUHA Impex wana nambari ya leseni 0005. Kampuni nyingine MCAG wana leseni namba 0006. Matle Investiment Company LTD wana leseni nambari 0007, Shoppers Trading Ltd wana leseni namba 0008 na Kizota Agro Products Ltd wana leseni 0009, hizo ni baadhi ya kampuni zilizopewa leseni na Mamlaka ya Bodi ya Korosho, kwa ajili ya kununua na kusafirisha nje ya nchi zikiwa ghafi.

Baadhi ya wakulima wa zao la korosho wanaona bora waanze kulima ufuta na mtama kuliko kuendelea kulima zao la korosho ambalo linagharama nyingi za uzalishaji kuliko mapato yake. Walidai kwamba kila kukicha kunakuwa na vikao mbalimbali vya wadau wa zao la korosho lakini huwa mara nyingi hakupatikani ufumbuzi wa kudumu kwa mkulima.

Walisema vikao hivyo, vingi vya kisiasa zaidi kumlaghai mkulima siyo kwa ajili ya utekelezaji wake na kuona mkulima yuko huru na inapofika msimu wa zao hilo kelele zinazidi. Naye Mwenyekiti wa chama cha wakulima cha Mbwemkuru Athumani Singano alisema kuna tani 100 za korosho katika Kijiji cha Mbekenyera, wilayani Ruangwa.

Alisema kwamba tani hizo za korosho za wakulima zinanyeshewa na mvua kutokana kuzuiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kutouza mnadani, katika msimu wa mwaka huu. Singano alisema kwamba kila msimu wa mwaka wa zao hilo kunakuwapo na migongano baina ya vyama vya wakulima na mamlaka husika juu ya utaratibu wa ukusanyaji wa zao la korosho.

Habari Leo
 
kwa ufupi ccm haithamini watu wake, kwani kwenye makapuni hayo mafisadi waliojaa ccm ndio wanamoponea.
 
Shida ni kuwa serikali haikudhani kuwa watu wa Lindi na Mtwara wanaweza kugeuka chama tawala.

Waliamini kuwa huko ni ngome ya CCM na kukawa na ahadi hewa za kisiasa wakati wa uchaguzi. Kwa kuwa wananchi wanaona hali mbaya, sasa wamefikia point ambayo wanahitaji utekelezaji.

Wabunge wao nao hata kutunza tu mahusiano na watu wao ni shida.

Sehemu nyingine za Tanzania zilizoachwa nyuma kama Kigoma, tayari wameanza kuikataa kwa nguvu CCM, tuone huko Lindi na Mtwara.
 
Mtwara and Lindi are the zones that are taken for granted by CCM.

Watu wa Mtwara mjue hivyo. CCM inaamini inaweza kuwapuuza kwa namna zote na bado mkaichagua kwa kishindo.

Hiyo ndiyo zawadi ya mapenzi yenu kwa CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…