CCM Mbeya: Hatutamvumilia yoyote atakayeharibu mali za chama, kuanzia sasa watakaokodi uwanja wa Sokoine kupewa masharti maalumu

Diamond BABA LAO!!

"Kanyaga Kanyaga"

Hapo lazima wanakyusa waharibu pitch.
 
Viongozi wa CCM mbeya waache ushamba wa kusimama mbele ya vyombo vya habari na kusema ujinga wa kuwa hivyo viwanja nivya CCM.

Tukiweka uchumia vyama pembeni tukafuata iliyokweli;

Hivi Kuna Chama chochote Cha siasa Tanzania ambacho kinaweza kutumia pesa za wanachama wake kujenge viwanja vya mpira karibia kila mkoa?(Tena kwa Zama hizi za wanachama wengi).

Ukweli: Hivyo viwanja vyote vinavyomilikiwa na CCM nchini hazijajengwa kwa pesa ya wanaCCM Bali Ni pesa za watanzania wote. Hayo Mambo ya kujimwambafy kuwa Ni Mali ya Chama Ni uongo Mkubwa.
CCM Acheni unafiki. Watanzania tunaelewa Sana sema tunamezea tu.

Swali la kufungia mwaka;
KAMA CCM INGEKUWA NA UWEZO WA KUJENGA VIWANJA VYA MPIRA MBONA SASA HIVI HAIJENGI? JE VIWANJA VYA MPIRA TANZANIA VIMESHATOSHA?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…