Uchaguzi 2020 CCM Micheweni yalaani uchochezi wa ACT - Wazalendo

blix22

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2013
Posts
213
Reaction score
645
Naibu Katibu Mkuu wa ACT-WAZALENDO Nassor Mazrui alitoa matamshi yanayohamasisha ghasia mnamo tarehe 26.08.2020 akifuatiwa na Mwenyekiti wa chama hicho Maalim Seif ambaye alihamasisha vurugu tarehe 30.08.2020.

Kufuatia hatua hiyo, afisi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wilayani Micheweni imelaani vikali kauli za uchochezi zilizotolewa na viongozi wa ACT-WAZALENDO hivi karibuni.

Katika taarifa iliyotolewa na CCM kwa vyombo vya habari, Maalim Seif ametakiwa kutorejea uchochezi alioufanya mwaka 2001 ambapo watu kadhaa walipoteza uhai wao, wengine wakasalia wakimbizi huku watoto wakisalia kuwa mayatima na baadhi ya wanawake kuwa wakimbizi.

CCM inamtaka Maalim Seif kutorejea uhalifu alioufanya huku wananchi wakitakiwa kuendelea kudumisha amani.

Maalim Seif huchochea maandamano ya vurugu huku familia yake ikiwa bukheir nyumbani.

Kwa miongo kadhaa Maalim Seif amekua akitumiwa na mabeberu kuyumbisha amani ya Zanzibar kama njia ya kukwamisha maendeleo ya visiwa hivyo.
 
Haya Sasa. Dude limeamshwa huko Micheweni
 
Kila mtu ashinde mechi zake kihalali, mkileta tu figisu safari hii lazima kinuke, sasa basi inatosha.
 
Hakuna amani wala upendo pasipo na haki.
Sio kila kicheko ni furaha...
 
Mbona hao ccm wanaongea kama chombo cha dola?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…