Zanzibar 2020 CCM mmesahau kuwa kwenye dini ya kiislam kufa ukitetea wanyonge ni ushujaa

Zanzibar 2020 CCM mmesahau kuwa kwenye dini ya kiislam kufa ukitetea wanyonge ni ushujaa

puza46b

Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
91
Reaction score
261
Bila kuandika mengi, CCM watakipata wanachokitafuta Zanzibar. Wamesahau jukumu la Waislam katika kuitetea haki kama wanavyoamriwa na dini.

Wamesahau dini inasemaje kuhusu yule anayejitoa mhanga kuokoa wanaonyanyaswa. Waliuwawa 2001 wakanyamaza. Wamefungwa viongozi wao wa dini wakanyamaza.

Wameshatoa onyo kwamba na liwalo naliwe.
Narudia tena, vita ya Tanzania itaanzia Zanzibar.

Chonde chonde wazee wetu, Warioba, Kikwete, na yeyote yule anayeweza kuwazaba makofi viongozi wa CCM waamke waone hatari inayoikabili nchi.

Hii vita itakuwa ina udini, ukabila na ukanda.
Zanzibar kwa sasa ni kama kifaru kilichobanwa kwenye kona. Hakina pa kutokea zaidi ya kumvamia yule aliyemzibia njia. Hakuna atakayekuwa salama.

Hii post ni woga wangu na simanzi kwa nchi yangu. Nawaomba wana CCM muamke, hamtaimba hayo mapambio kikiwaka.
Hakuna mshindi ndugu wakigombana. Ila CCM mna mengi ya kupoteza kuliko upinzani.

Hivyo basi nawaombeni busara zenu ili hichi kikombe kitupitie mbali.

Sent from my SM-G935W8 using JamiiForums mobile app
 
Sikio la kufa halisikii dawa

Mungu aliufanya mgumu moyo wa farao ili kweli na haki idhihilike.

CCM ni sikio la kufa na Mungu ameujaza moyo wa ufalme kiburi.
 
Uchaguzi huu naiona "things fall apart"
lla sivyo CCM wakubali kukabidhi madaraka kwa wapinzani
 
Nashangaaa sana Eti Sirro na yule mpuuzi awadh anawatishia waislamu kufa na kupigwa?????

Nafikiri hawa watu warudi kwenye mitandao wasome Kwa nini Arab Spring ilifanikiwa 2010 - 2011.

Kwa kifupi muislamu atishiwi kupigwa wala kuuwawa kwa sababu ukifa ukitetea haki katika uislamu unaipata pepo!!

Ninachokiona mwaka huu ni polisi kufanya na vyombo vya usalama kufanya mauaji na hapo mwaka kesho wakuu wa polisi na usalama Zanzibar na bara kutokewa arrest warrant na ICC tena wakiongozwa na Jiwe mwenyewe!
 
Ni makosa makubwa Sana na kumkufuru Mola kwa muislamu kuirudisha tena ccm madarakani ili ije ikuteseni Tena.Musiba angekuwa ni muislamu siku nyingi Sana angeshaozea ndani. Muislamu akitoa mawazo yake anawekwa ndani. Nini cha kunufaika nacho sasa
 
Acheni propaganda tunahitaji amani
 
Kama unaona kufa ni ushujaa si ujinyonge peke yako?

2001 walinyamaza kimya au walinyamazishwa?

Hiyo chuki dhidi ya wanaowatakia mema ndiyo inayosababisha dhambi hiyo kuwatafuna.

Mungu hapendi hayo mafarakano yatawaathiri sana mtaicha Dunia na Dunia lazima iendelee.
 
Ccm wanaweweseka Sana maana wanajua hawawezi kushinda uchaguzi wowote huru
 
Funga kazi leo mgombea Urais wa CCM Zanzibar watu wamemwachia msikiti baada ya kuingia , wasema hawawezi kuswali na mnafiki mwaka huu CCM wataipata .
 
Kama unaona kufa ni ushujaa si ujinyonge peke yako?

2001 walinyamaza kimya au walinyamazishwa?

Hiyo chuki dhidi ya wanaowatakia mema ndiyo inayosababisha dhambi hiyo kuwatafuna.

Mungu hapendi hayo mafarakano yatawaathiri sana mtaicha Dunia na Dunia lazima iendelee.
Waambie CCM kwanza halafu rejea hapa. Mleta mada ana jambo la msingi wewe unaleta utani?
 
CCM ni sikio la kufa na Mungu ameujaza moyo wa ufalme kiburi
Mara nyingine mnapoandika mujuwe si kila msomaji anajua sarakasi zenu-----eleza ccm wamekosea nini ili na sie neutral tujue
 
Funga kazi leo mgombea Urais wa CCM Zanzibar watu wamemwachia msikiti baada ya kuingia , wasema hawawezi kuswali na mnafiki mwaka huu CCM wataipata .
Haya tielezeni unafki wake ni nini?, Au wao ndo wanafki?
 
Ndio maana inahitajika Cuf ili kuondoa zile kero zote wanazopata waislamu.
 
Uchaguzi huu naiona "things fall apart"
lla sivyo CCM wakubali kukabidhi madaraka kwa wapinzani
Kwahiyo huko kwenu wapinzani wameshashinda?, Mlikuwa na haja gani sasa kujaza fomu ?
 
Back
Top Bottom