CCM mnafikia hatua ya kuwafikisha Kinana, Makamba kamati ya Nidhamu? Hakika huko mnakoenda mwisho wake sio mzuri

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Nimeangalia sana mwenendo wa CCM ya leo na viongozi ambao wana historia nzito sana katika CCM na Tanzania kwa ujumla, na kufikia muafaka kwamba safari ya CCM kwenda huko wanakojua wenyewe mwisho wake sio mzuri.

Tangu uongozi wa CCM ya sasa uingie madarakani umekorofishana na karibu viongozi wote ambao huko nyuma walikuwa ni watu wenye heshima zao kubwa sana ndani ya chama.

Nakumbuka hii ni kuanzia Kingunge, Nyalandu, Prof. Mwandosya, Makamba, Membe, na Kinana! Na hata wamekua wakimchokonoa sana Kikwete, wengine kudiriki kumkosea heshima kwa kauli kwamba hakuna alofanya kulinganisha na Magufuli - kauli ambazo tungetegemea zitoke kwa watu wa vyama vya upinzani.

Hivi katika uzito wa kisiasa wa mtu kama Kinana, Makamba, leo hii ungetarajia waitwe hadharani kuhojiwa na Kamati ya Nidhamu ya CCM? Na jambo moja kubwa, hivi hawa wazito wa zamani wa CCM wanakorofishana na CCM kama chama au kiongozi mmoja tu ambaye mkipishana kauli anataka ionekane ionekane umeikorofisha CCM yote?

Nyie CCM huko mnakokwenda, au kwa usahihi zaidi, huko mnakopelekwa mwisho wake sio mzuri. Mark my words.
 
mkuu unayashtua ya nini!?? yaache yavurugane kwani kifo chao kitaleta faida kw mnyonge wa kweli wa nchi hii.!
 
Mkuu unauhakika kwamba huwashwi? Pinda ndiye mwenye sifa ya kukaa kimya (asiyewashwa)!
 
CCM haogopwi mtu tofauti na ukambale wa Chadema!
 
Hakuna mwanadamu asie na makosa.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuitwa kuhojiwa kwa viongozi haimaanishi kwamba Kuna tofauti, hapana, pengine Kuna Mambo wanataka kuwekana sawa.

Pia, ndani ya CCM ya sasa Ina uwezo wa kumuita hata mwenyekiti kumhoji kama Kuna Mambo wanaona hayaendi sawa.

Kinana na Makamba walitumikia chama chetu na nchi yetu lakini haimaanishi walikuwa wakubwa kuliko CCM au nchi hivyo kuitwa kuhojiwa ni kudhihirisha nisemacho
 
Kinachokuuma nini? Si ungependa CCM ife ili ninyi mchukue serikali?
 
Kwaio ungependa iendelee kulea ujinga kisa taito ya mtu. Hii ndio Safi hata huyu akimaliza muda wake Kama Kuna madudu alifanya ashatakiwe tu.
 
CCM haogopwi mtu tofauti na ukambale wa Chadema!
Mwambie huyo boya , Lowasa alikuwa na nguvu Sana CCM hao hao akina kinana , membe , na makamba ndo walimdrop down , JPM hakuwa na nguvu yyte and he came into power , somtyme mambo huwa upside down, kiufupi JPM nothing to fear cse yupo pale accidentary ,nan hajui Dr Slaa, mtei walikuwa wafuasi waaminifu wa CCM ?? CCM ina misingi yake dhabiti usishangae hata huyo JPM after 10 yrs anakuwa mdogo kama pirton
 
Tangu Sophia Simba anyang'anywe kadi ya CCM na kisha kurudishiwa kwa shingo upande niliamini CCM awamu ya 4 Pwani wamepatikana.
 
Sahihi kabisa

Azimio la Arusha watu walianza kufungia Vitumbua Nyerere akiwa hai wakati mwenyewe anakwambia kila akirudia kulisoma haoni pa kurekebisba walau koma


Jakaya kazomewa kwny NEC ya mwisho akiwa bado Amiri jeshi

Ccm ni chama cha aina yake sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Africa nzima hakuna chama bora kama CCM kuna vyama kibao itabidi vijifunze sana.
 
Kwani kuna ccm siku hizi au kuna policcm + wasiohulikana??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…