CCM mnafikia hatua ya kuwafikisha Kinana, Makamba kamati ya Nidhamu? Hakika huko mnakoenda mwisho wake sio mzuri

[emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419][emoji419]

Hit direct to the Ntonku
 

Hoja yako ati: Nyie CCM huko mnakokwenda, au kwa usahihi zaidi, huko mnakopelekwa mwisho wake sio mzuri, je, huko kwenye vyama vya upinzani ambako viongozi wake, wanachama, wameshona midomo yao wakati kuna maovu, ufisadi na kuminywa kwa demokrasia, utajuwa na hoja gani?

Moja ya misingi mikuu ya CCM, Cheo ni dhamana. Kwa msingi huo, chama, kama Taasisi, kiko juu ya hali, wadhifa na ukuu wa mtu mmoja mmoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sipo ccm sijui hata wanaopareti vipi mambo yao. Kifupi kwenye siasa mm ni shabiki tu.
Hamna kitu mbaya kwenye siasa kama kuwa shabiki - maana inabidi ushabikie hata ujinga ili mradi unashabikia japo kuna watu watakuona mwendawazimu.

Lakini pa, hakuna kitu hatari katika siasa kama kuwa mtu wa hoja, maana ukitoa hoja zinazotishia maslahi ya walioshika hatamu utafanywa kitu mbaya na hata kuuwawa.
 

Hapa tunaongelea CCM na suala la Kinana na Makamba. Sasa unataka niwaingize upinzani kwenye hii thread? Tafuta thread nilizoandika za watu wa upinzani ndio ukaone hoja zangu, lakini kwenye hii thread tunaongelea CCM. Kama huna point kaa kimya.
 
Hapa tunaongelea CCM na suala la Kinana na Makamba. Sasa unataka niwaingize upinzani kwenye hii thread? Tafuta thread nilizoandika za watu wa upinzani ndio ukaone hoja zangu, lakini kwenye hii thread tunaongelea CCM. Kama huna point kaa kimya.
CCM ni Taasisi imara kama chama cha siasa na ndiyo maana hakuna mwachama aliye juu ya chama. Mwanasiasa hupata umaarufu kupitia chama na si vinginevyo.
 
Musiba ndio mchonganishi na anatumwa
Cha ajabu zaidi ni kuwa wao CCM wanajua kiini cha yote yaliyotokea ni huyo mtu wanayemwita Musiba, kuwachafua watu bila ushahidi na kuachiwa afanye atakalo.......

Hao wazee walipohoji tu kuwa inawezekanaje mtu mmoja Musiba, anaendelea kuwachafua na kuwatukana watu hadharani bila kuchukuliwa hatua?

Ndiyo hayo yaliyowakuta kufukuzwa kwenye Chama!

Hakika hivi sasa chama hiko kikongwe kabisa barani Afrika, kipo katika hatua ya "The last kicks of the dyeing horse"
 
Wapumbavu wanashangilia upinzani utakufa hawajui upinzani unahamia ndani ya chama chao,mheshimiwa anatengeza ccm yake hao wanao sajiliwa hawaipendi ccm wanampenda mwenyekiti aliye wasajili na walikotoka hawatakiwi tena wanacho fanya sasa ni kumfia mwenyekiti adumu milele,kibaya zaidi wanapewa platform,au speaker tena za upendeleo yaani wana kuwa maDC,Makatibu tawala,mawaziri wabunge,hawa ndiyo askari watakao pindua katiba na kuonekana ccm unataka hayo ili jamaa aongeze muda,CCM wapo kwenye vita lakini hawajifahamu,matumbo yamewatia upofu wako tayari kumwabudu shetani kwa ajili ya shibe,wamesahau nguvu kubwa walioitumia kwa miaka mingi kukijenga chama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…