Ccm mnalo babu...!

mcfm40

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
4,452
Reaction score
3,151
Ndugu Wananchi,
CCM haitaki serikali tatu, inataka mbili. Lakini hawajui hiyo mbili waikarabatije ili ikubalike. Ni hivi. CCM wapo kwenye mtego mkubwa kabisa kuwahi kutokea katika historia yao. Wazanzibari wamebadili katiba yao na katika kubadili huko wakavunja katiba ya muungano. Hakuna mwanaCCM yeyeote aliyedhubutu kuwaambia ukweli kwamba wamekosea. ikwete na wenzake waliapa kulinda na kuitetea katiba ya jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini imevunjwa mchana kweupe. Wanachokisema wao (kina Werema na Samaia suluhu) ni kwamba mabadiliko hayo hayana madhara kwa muungano!!! Really!

Mpaka leo binafsi sielewi inakuwaje hakuna kesi yoyote mahakamani ya kuishitaki zanzibar kwa kuvunja katiba ya jamuhuri ya Muungano wa tanzania na kufanya katiba yao kuwa juu ya Katiba mama?? Hebu nijuzeni waungwana kwa nini miaka minne sasa bado sioni kesi yoyote kuishitaki zanzibar na hata pia serikali ya jamuhuri ya muungano kwa kushindwa kulinda katiba waliyoapia kuilinda na kuitetea?? hebu nitegulieni kitendawili hiki tafadahali.

Turudi kwenye kujitega kwa CCM. Kasheshe ipo hapa sasa kwenye bunge la katiba na serikali tatu. CCM wana option ya kukubali serikali tatu au kungangania serikali mbili (ambapo sioni km bunge la katiba litaendelea km sisiem watakomaa na msimamo wao huo; maana yake itabidi itungwe rasimu mpya kabisa na sioni km itawezekana). Tuseme wamengangania serikali mbili na bunge likaendelea bila kuvunjika maana yake itabidi (CCM) wawalazimishe zanzibar wabadilishe vipenge vya katiba yao km mwanakijiji alivyoeleza ili mantiki ya serikali mbili iwepo.

Swali, Je ndugu wananchi, mnadahni CCM wanaubavu wa kuwalazimisha zanzibar kubadili katiba yao? ...Si wanaogopa kuwaudhi wasije wakajitoa kwenye Muungano? je mnadhani wazanzibar watakubali kufanyia marekebisho katiba yao ( hapa pia ikumbukwe kwamba lazima iitwe referendum ili wananchi wayakubali mabadiliko, ndivyo katiba yao inavyosema.)
Kufanya marekebisho hapa maana yake ni kutoa vile vifungu vinavyoipa zanzibar mwelekeo wa kuonekana km vile inajitegemea, ni mamlaka kamili. Alas, vifungu hivi ndivyo hasa wanzanzibar wanavipigia chapuo na wanataka zaidi ili wawe na mamlaka ya kujiamulia wenyewe.

Hakika CCM mnalo mwaka huu. hamna namna ya kutoka kwenye hii dillema. Kila njia ya kutokea ni ya kuendea kifo. Mnalo nawambia. israel kwangangania lazima aondoke na roho ya mtu. Hii tamthiliya ya katiba ni tamu jamani hebu tusubiri tuone watajitoaje kwenye huu mkanganyiko.

Binafsi mimi nasema hakuna katiba mwaka huu. Ikiwa kinyume chake nitatoa laki moja kwa jamii forum, la sivyo nipigwe life ban.
 
wewe unafikiri misukule kama Ole Sendeka,Ummy Mwalimu,pindu Chana watakuelewa.
 
Nawasikitikia sana magamba.miti yote inateleza
 
Nawasikitikia sana magamba.miti yote inateleza

Ngoja tuone watakavyojichanganya. Wale wazanzibar waliokuwa na moto sana wakati wa ile sheria ya katiba siku hizi wapo kimya sana. Jamani zanzibar mitaani huko mnazungumza katiba au ndio mmeshaipotezea?
 
WaZanzibari wapo CooL kabisa hawana wasiwasi wanakula mbatata za ulojo na jioni wanaenda kwenye Taarabu ,wanajua fika WaTanganyika hawataipoteza Chance ya kurudisha Nchi yao.
 
WaZanzibari wapo CooL kabisa hawana wasiwasi wanakula mbatata za ulojo na jioni wanaenda kwenye Taarabu ,wanajua fika WaTanganyika hawataipoteza Chance ya kurudisha Nchi yao.

CCM inawaogopa wazenji kweli kweli! Ila nao wazenji wapambane si unaona wale wanaotoka CCM wanasema wazanzibar wanataka serikali mbili? Je eti mmewatuma hivyo au wanawasemea wanayofikiri wao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…