Bowie
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 4,373
- 6,084
Toka tupate Uhuru 1961 Tanzania imetawaliwa na Tanu na baadaye CCM lakini cha kusikitisha ni jinsi ya uchumi wa Tanzania unavyoendeshwa kwa njia tofauti katika utawala wote wa awamu sita.
Awamu ya kwanza njia zote za kiuchumi zilithibitiwa na serikali na utaifishaji mkubwa wa majumba/mashamba/biashara kubwa ulifanyika. Ilianzishwa mashirika ya serikali kama RTC, National Milling, Kabimita etc . Sera hiyo ya kiuchumi ilishindwa kabisa.
Awamu ya pili ilikuwa ni awamu ya ruksa ambapo serikali ilijitoa katika masuala ya kufanya biashara na biashara ikawa huria lakini ukusanyaji wa kodi ulikuwa mbovu sana.
Awamu ya tatu ilikuja na sera ya ubinafishaji ambapo tuliona mabenki na viwanda vikibinafishwa kwa bei chee na mfumo wa biashara huria uliendelea.
Awamu 4 Ulikuja na mikakati ya njia mbadala wa kutumia Gesi kama uzalishaji wa umeme na mabilioni ya fedha yalikopwa ili kujenga bomba la gesi kutoka kusini mpaka Dar. Mradi wa kujengwa bandari ya Bagamoyo ulianzishwa.
Awamu ya 5 Ulingia madarakani na kuacha mradi wa umeme wa gesi na kuamua kuingia kwenye mradi mkubwa wa umeme kwa kutumia maji.
Stiegler's Gorge project na mpaka sasa haujakamilika. Mradi wa treni wa standard gauge ulianzishwa pia. Sekta binafsi zilikuwa na wakati mgumu sana kipindi cha awamu hiki kwa kubandikiwa kodi na hii ilipelekea biashara nyingi kufungwa na wawekezaji kukimbia. Mradi wa kujenga Bandari ya Bagamoyo ulisitishwa.
Awamu ya sita Sekta binafsi imepata afueni na wawekezaji wameanza kurudi na mradi wa Ujenzi wa bandari ya Bagamoyo umeanza kuzungumzua upya.
Kwanini CCM isiweke Road Map kwenye masuala ya uchumi wa Tanzania ili kila awamu ifuate sera moja katika kujenga uchumi. Hii itasaidie wafanyabiashara na wawekezaji kuwa na imani serikali yeyote ya CCM katika kufanya biashara Tanzania