Pre GE2025 CCM Morogoro waonyana tabia ya makada kuanza kampeni kabla ya muda elekezi. Mjumbe wa kamati kuu atoa neno

Pre GE2025 CCM Morogoro waonyana tabia ya makada kuanza kampeni kabla ya muda elekezi. Mjumbe wa kamati kuu atoa neno

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Morogoro kimewataka wanachama wa chama hicho pamoja na watia nia katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu kuacha kujishughulisha na kampeni za uchonganishi ambazo tayari baadhi ya watu wamedaiwa kuanza kupita mtaani kuomba kura badala yake wasubiri wakati sahihi.

Akizungumza hayo Jonas Nkya Mjumbe wa kamati kuu ya taifa CCM (NEC) alipokuwa katika mkutano wa maadhimisho ya miaka 48 ya CCM yaliyofanyika Wilaya ya Kilosa Morogoro.

Soma pia: Mwenyekiti wa CCM Morogoro awapiga biti kali wagombea walioanza kampeni kabla ya muda uliopangwa

Aidha Nkya amesema kuwa sio busara kutoa maneno machafu kwa watu kwa lengo la kumharibia mtu badala yake kila mtu asimame katika mtazamo ulio chanya lengo ni kuitengeneza Tanzania Imara


 
Back
Top Bottom