Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Morogoro kimewataka wanachama wa chama hicho pamoja na watia nia katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu kuacha kujishughulisha na kampeni za uchonganishi ambazo tayari baadhi ya watu wamedaiwa kuanza kupita mtaani kuomba kura badala yake wasubiri wakati sahihi.
Akizungumza hayo Jonas Nkya Mjumbe wa kamati kuu ya taifa CCM (NEC) alipokuwa katika mkutano wa maadhimisho ya miaka 48 ya CCM yaliyofanyika Wilaya ya Kilosa Morogoro.
Aidha Nkya amesema kuwa sio busara kutoa maneno machafu kwa watu kwa lengo la kumharibia mtu badala yake kila mtu asimame katika mtazamo ulio chanya lengo ni kuitengeneza Tanzania Imara