Papaa Mobimba
JF-Expert Member
- Jan 27, 2018
- 882
- 3,337
Kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, kimetoa rai kwa wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
Hayo yamebainishwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Mvomero Florance Machicho wakati wa sherehe za siku ya mwanamke Duniani sherehe zilizoenda sambamba na ugawaji wa taulo za kike kwa wanafunzi kutoka katika Wilaya hiyo.
Baadhi ya Wanawake kutoka katika Wilaya hiyo wamesema kwa sasa wanauelewa mkubwa kuhusiana na masuala ya kisiasa.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025