Uchaguzi 2020 CCM mwaka huu wa uchaguzi muwe wapole na wastaarabu, tofauti na hivyo mtatusababishia machafuko makubwa

Uchaguzi 2020 CCM mwaka huu wa uchaguzi muwe wapole na wastaarabu, tofauti na hivyo mtatusababishia machafuko makubwa

nguruka wa kig0ma

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2020
Posts
2,946
Reaction score
2,932
Nina maono ya mbali sana wanabodi.
Ninamwona Mh Lissu akiwa na nguvu kubwa ndani na nje ya nchi

Namwona akibebwa na wananchi wengi,
1. Wasomi, hawa wanampenda kwakuwa waneuona ukweli na uwazi kwake.
Wameona ni mtu wa kulinda katiba ya nchi ivyo ataiongoza nchi kwa katiba, na atarudisha mchakato wa katiba mpya ambayo wengi wanamatumaini nayo kwa mustakabari wa taifa.

2. Namwona akibebwa na vijana wengi, wanaotazamia ajira Serikali na wale waliokuwa wakifuatilia hoja zake na utetezi wake bungeni

3. Wananchi wa vijijini hasa wazee wa kike na kiume.
Hawa hawakuzoea kuona wanasiasa wakipigana risasi kwa kusudio la kuuana,
Hivyo tukio lile limewatia huruma na uchungu mkubwa juu ya Lissu, kama wazazi, hasa wakizingatia lissu hakuwa na makuu na msema kweli

4. Nimeona akibebwa na mataifa makubwa duniani,
Kupigwa kwake risasi na kukaa kwake nje kwa muda mrefu, amekuwa kama waziri wa mambo ya nje wa tanzania.
a) kupigwa kwake kumeyaudhi mataifa hayo.
b) kujieleza kwake vizuri juu ya democracy ya tanzania, kumeiweka uchi nchi yetu kiasi kwamba mataifa hayo yameichukia ccm

c) Mahusiano mabaya ya uongozi wa nchi yetu na mataifa hayo ya magharibi na vita vya kiuchumi baina ya magharibi na china, hasa Marekani.
Hawa hawatataka ccm iendelee kuongoza.
Hivyo ushindi kwa Lissu ni dhahili.

My take
Nawaonya CCM, iweni wapole kama hua ili baada ya uchaguzi nchi iwe salama.

Ninyi hamna kibali cha milele kuongoza nchi hii.
Chochote mtakachofanya cha dhulma kwa kutumia vyombo vyenu vya ulinzi na usalama ili mshinde kitatuletea taabu ambayo hatutaisahau milele

Kumbukeni kuwa humu nchini wamo wazazi wenu watoto wenu, bibi zenu, shangazi zenu, binamu zenu nk.
ACHENI HAKI ICHUKUE NAFASI ILI AMANI UTULIVU VIWEPO.
Karibu
 
Tatizo sio lissu tatizo hamjaanda watu makini balaza la mawaziri pia me naona uyu lissu anabebwa na Huruma kutokana na alichofanyiwa ila sio kwa kuwa rais wa nchi.....adi kufikia sasa yupo nje ya nchi bado tunaendelea kumuamini tu? Ebu tufikilie mbele maisha yanaenda kasi sana
 
Msipange kuchafua uchaguzi mkasema ni CCM, kipigo Cha mbwa koko kwa upinzani kipo palepale.
 
Hapa najiuliza Green guard wamejiandaa kufanya nini maana.... duu

Ila yote na yote kuuana isiwe ajenda kabisa tushindane kwa hoja tu.
 
Acha kuota mchana huu nenda katafute chakula cha mchana.
Huyu Lissu anapendwa labda na mashoga anaowaunga mkono na acha kuwasingizia watanzania mambo ya kijinga tafadhali sana

Watanzania wengi wana imani na rais wao mpendwa JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI. [emoji1241]

Tayari amekwisha onyesha dira ya muelekeo wa taifa letu.
Ila kwa majizi na walilia madaraka ili waendelee kuiba kama zamani ndio hamtaki kuamini, kusikia wala kumuona akiendelea kupaa
 
Hata Babu alikuwa kijana,Ila muda wake wa ujana umekwisha pita
 
Back
Top Bottom