Izack Mwanahapa
JF-Expert Member
- Apr 21, 2011
- 497
- 236
Mitazamo ya CCM na CHADEMA kuhusu mapendekezo ya mfumo wa serikali kwenye Rasimu ya katiba mpya inafanana kabisa. wote wamelenga maslahi ya vyama vyao na si maslahi ya wananchi. Kila chama kinataka idadi fulani ya serikali kwa maslahi ya chama husika, vita ya maneno inayoendelea hivi sasa kati ya CCM na CHADEMA haina tija. Wawili hawa wanatunishiana misuli kwa lengo kuona nani mbabe kichama bila kujali mwananchi ananufaikaje. Ni vita ya viongozi wa vyama wanaopigania maslahi ya yao kupitia ushabiki wa wananchi.
Tusidanganyane hakuna nchi yoyote iliyoendelea duniani kwa kuwa na utitiri wa serikali kwa mkupuo. Kwa hali ilivyo katika nchi yetu hivi sasa serikali tatu au serikali mbili ni mzigo kwa wananchi. Ili tuendelee Nchi hii inahitaji serikali moja yenye uongozi makini iwe kwa kuungana au kwa kutokuungana na Zanzibar.
Ila katika mjadala huu wa idadi ya serikali Kinachosikitisha ni kwamba mawazo halisi ya watanzania walio wengi yamemezwa na misimamo na mitazamo ya vyama vyao. Kwani wengi husapoti kishabiki chochote kile kitakachosemwa na kiongozi wa chama chake kwa kudhani kuwa wanakikomoa chama au vyama vingine kumbe wanajikomoa wenyewe.
Katika hali hii ya njaa kali kwa wanasiasa wetu wa vyama vyote, wananchi tunatakiwa kuwa makini katika kuangalia, kusimamia na kuhoji mambo yote ya msingi yanayotuhusu. Tusiache viongozi wa vyama watuburuze kwa maslahi yao binafsi kwani "Kamwe Paka hawezi kujifunga kengele ili panya wamkimbie kabla hajawafikia".
Ni muhimu kujua sababu zako binafsi za kuunga mkono jambo fulani, bila kufanya hivyo tutakuwa tunawaunga mkono watu badala ya kuunga mkono hoja za msingi. Kama unadhani utitiri wa serikali una tija tupe mfano wa nchi iliyoendelea kwa staili hii ya serikali zinazopendekezwa.