CCM na CHADEMA mnaharibu mchakato wa katiba mpya

CCM na CHADEMA mnaharibu mchakato wa katiba mpya

Lilambo

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2013
Posts
2,523
Reaction score
207
Naomba niweke wazi, vyama hivi viwili vimekuwa vikishawishi wananchi na wanachama wake kupendekeza maoni yenye maslahi kwa vyama vyao.

CCM wamejikita kuwaeleza wanachama mtazamo wao kama chama na kushawishi watu.

Pia kwa upande wa cdm mikutano wanayoifanya wanawashawishi watu kupendekeza maoni yanayoibeba CHADEMA.

Mfano ni ktk serikali tatu, CHADEMA wanaamini CCM huwa inashinda kupitia kura za wazanzinbar hivyo CHADEMA wanataka gvt tatu ili waweze kuinhia Ikulu kwani kura za zanzibar hazitokuwepo.

CCM wanadai wanadai serikali mbili ili´kura za wazanzibar ziendelee kuwaweka Ikulu.

Kwa mtazamo huu, Vyama hivi havimtzami mtanzania wa chini bali vinatafuta njia ya kuingia Ikulu tu.

Watanzania tutaendelea kubaki nyuma kwani katiba hii haitatusaidia kwani kusaidia vyama vya siasa.
 
Kwa jinsi Mchakato unavyoendelea sidhani kama tutapata Katiba yenye Manufaa kwa Mtanzania.
 
Hapa nani anayeharibu mchakato; anayekataa kifungu kilichopendekezwa Na tume ya katiba au anayeunga mkono?

Naona hapa umeandika ili u balance, lakini you are wrong. Chadema haipingi Na haijakataa mapendekezo ya tume bali CCM ndio inayopinga Hivyo CCM ndio inayotaka kuharibu mchakato
 
Warioba kamaliza utata, taarifa ya habari itv, kasema hawatapokea maoni ya majukwaani. Wanataka maoni ya mwananchi na siyo ya kutumwa na mwanasiasa.
 
Back
Top Bottom