CCM na CRC - Chama tawala Comoro kushirikiana

CCM na CRC - Chama tawala Comoro kushirikiana

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi amekutana na Mheshimiwa Youssoufa Mohamed Ali, Waziri wa Ulinzi ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama Tawala Comoro cha CRC ambaye pia ni Katibu wa Rais wa Umoja wa Visiwa vya Comoro na kuzungumzia kuimarisha uhusiano baina ya vyama hivyo ikiwa ni pamoja na kutoa fursa za mafunzo kwa watendaji wa Chama cha CRC nchini Tanzania.
IMG-20241103-WA0049.jpg

Aidha viongozi hao wamepongeza juhudi za ushirikiano wa nchi hizo mbili unaofanywa na Marais wake Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan na Mheshimiwa Azali Assoumani.
IMG-20241103-WA0053.jpg

Ziara hiyo imeratibiwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro, Mheshimiwa Youssoufa anatarajiwa pia kutembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Shirika la Uzalishaji Mali SUMA JKT na pia Taasisi binafsi kadhaa zenye dhamira ya kuwekeza nchini Comoro.
IMG-20241103-WA0051.jpg
IMG-20241103-WA0055.jpg
 

Attachments

  • IMG-20241103-WA0057.jpg
    IMG-20241103-WA0057.jpg
    444 KB · Views: 7
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amekutana na Mhe. Youssoufa Mohamed Ali, Katibu Mkuu wa Convention for the Renewal of the Comoros (CRC), chama tawala nchini Comoro.

Mazungumzo hayo ya pande mbili, yaliyohusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya vyama hivyo, serikali na nchi hizo mbili kwa ujumla, yalifanyika katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam, tarehe 2 Novemba 2024.

Mhe. Youssoufa Mohamed Ali, ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na Katibu wa Rais wa Comoro, yupo nchini kwa ziara ya kikazi inayoendelea kuanzia tarehe 2 hadi 5 Novemba 2024.
IMG-20241103-WA0022.jpg
IMG-20241103-WA0020.jpg
IMG-20241103-WA0018.jpg
IMG-20241103-WA0016.jpg
 

Attachments

  • IMG-20241103-WA0014.jpg
    IMG-20241103-WA0014.jpg
    424.9 KB · Views: 3
  • IMG-20241103-WA0012.jpg
    IMG-20241103-WA0012.jpg
    496.3 KB · Views: 4
  • IMG-20241103-WA0010.jpg
    IMG-20241103-WA0010.jpg
    516.5 KB · Views: 5
  • IMG-20241103-WA0006.jpg
    IMG-20241103-WA0006.jpg
    516.3 KB · Views: 3
Back
Top Bottom