Watanzania
JF-Expert Member
- Jul 7, 2009
- 727
- 44
Kati ya urithi mkubwa aliotuachia baba yetu wa taifa Mwl. Nyerere ni umoja wa kitaifa. Umoja huu haukuja kama mvua bali alijenga misimgi imara ya kudumisha umoja wetu. Moja ya misingi hiyo ni kutoingiza udini na ukabila katika uongozi, serikali na siasa za nchi yetu.
Mwalimu Nyerere alisema huku akishikashika pua kama kawaida yake anapoongea suala zito kuwa, mwanasiasa aliyefilisika kisiasa hukimbilia udini na ukabila ili aungwe mkono. Miaka sita tu baada ya kifo cha mwalimu Nyerere, CCM imefanya kituko cha mwaka kwa kuingiza masuala ya dini ya kiislam- Mahakama ya kadhi katika ilani yake ya uchaguzi. Kwa kufanya hivi CCM wamedhihirisha kufilisika kisiasa kwa vile wanatafuta sasa kura za kidini huku wakijua kuwa ni kuiangamiza nchi yetu.
Tunajua wazi kuwa mahakama ya kadhi inahusika na mambo ya ibada za kiislam. Mashehe wameshasema kuwa mtume wao aliwafundisha kuwa mahakama ya kadhi inahusika na mambo ya ibada ndiyo maana watu wa dini nyingine hawatakiwi waamue masuala yao. Kumbe CCM na waislam wanajua kuwa mahakama hiyo inahusika na masuala ya ibada za kiislam, kwa nini sasa wanataka iiendeshwe na wananchi wote kwa kulipa kodi na kuingizwa katika sheria za serikali kana kwamba nchi yetu ni ya dini ya kiislam? Mambo ya ibada yanatakiwa yaendeshwe na waislam wenyewe na siyo serikali wala wananchi wote.
CUF nao kupitia mwenyekiti wao Lipumba anasema eti CCM watekeleza kipengele cha mahakama ya kadhi huku akijua kuwa ni kuingiza masula ya ibada ya dini ya kiislam katika shughuli za serikali. Masuala ya mfungo wa ramadhani, ndoa na mirathi yamefungamana na ibada za kiislam. Ramadhani ni nguzo ya dini ya kiislam na ndoa za waislam zinaruhusu wake wengi, wakati dini nyingine hasa wakristo wanaamini katika mke mmoja. Sasa kwa nini CCM inataka kuwalazimisha watanzania wote hata wasio waislam washiriki ibada za kiislam ili tu wapate kura?
Mbunge Msambya nae anadhani yuko bungeni kueneza dini ya uislam, na anafikiri anawakilisha bungeni waislam pekee. Ngasongwa naye anatumika kuingiza udini katika ilani yaCCM pamoja na usomi wake.
Kwa kukumbatia udini CCM na CUF wamefilisika kisiasa na hawastahili kura zetu kwa sababu watatuletea utengano katika taifa letu na hivyo kuvunja umoja alioujenga baba yetu wa taifa.