Huyu umalesso kweli ni lesso, mbona wakristo wao hawajadai na hawafaidiki na mhiyo KODI, KWANI nani hataki kufaidika na hizo kodi--------acha kuwa lesso bwana.
Mimi ni MwanaChadema na nashauri viongozi wangu watamke kwamba hawapingi kuwepo kwa Mahakama ya Kadhi. Sharti moja muhimu ni kwamba MYK iwe ni taasisi isiyokuwa ya kiserikali yaani Non-Governmental Organization na finances zake zitokane na zakat na wafadhili wengine wa ndani na nje.
Narudia maelezo yangu ya awali kwamba Wakristo wengi wanatumia vikao vya Kanisa kutatua matatizo ya ndoa zao. Watanzania wengi wanatatua matatizo yao ya MIRATHI kwa kutumia vikao vya ukoo. Hivi vikao havilipiwi na Serikali.
Narudia pia kwamba Katiba ya Tanzania Ibara ya 19(2) inatamka wazi wazi kwamba mashughuli yote ya dini yatakuwa ni mambo ambayo hayatalipiwa na fedha za serikali. Ni kinyume na Katiba kwa Bunge kupitisha Bajeti itakayolipia MYK.
Maoni yangu ni kwamba itakuwa ni jambo la kizalendo sana kama kutatokea MwanaJF kujitoa hadharani kwenda Kortini juu ya uvunjifu huu wa Katiba. Niko tayari kumchangia.