Deogratias Mutungi
Senior Member
- Oct 1, 2019
- 140
- 181
Nawasalimu Wana JF
Nawajulisha kuwa nimefatilia kwa karibu sana mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama cha Mapinduzi CCM kwa ngazi ya Wenyeviti na Wajumbe wake uliomalizika usiku wa kuamkia jana. Kutokana na tafiti zangu nimegundua CCM ni miongoni mwa vyama vya siasa hapa nchini vyenye mfumo dhabiti na wa kidemokrasia katika kuwapata wagombea wake. Mantiki ninayoikusudia hapa kuiwakilisha kwenu ni Mfumo wa demokrasia ndani CCM ambao nimeuona kuwa nguzo pekee inayoendelea kukifanya chama hiki kiendelee kuaminika na kushika dola.
Sababu za hoja zangu zipo wazi na zinajikita katika haki na kufata katiba ya chama chao. Mfano;
(i) Wagombea wote walio shindwa kuleta maendeleo majina yao yalikatwa ngazi ya Wilaya.
(ii) Waliokuwa na makundi majina yao yalikatwa ngazi ya Wilaya.
(iii) Waliotoa rushwa na kufanya kampeni kabla ya wakati nao walikatwa kwa mujibu wa taratibu za chama.
Funzo ni nini hapa? Wanasiasa na Wana CCM wajifunze kuwajibika na kuleta maendeleo kwa wananchi aidha watambue CCM si hati miliki ya mtu bali taasisi ya watu inayojikita kwenye haki na demokrasia ya kweli.
Ni rai yangu kwa vyama vya upinzani kujifunza kwa chama hiki kikongwe ili kuweza kuleta ushindani wa kweli ndani ya siasa zetu hapa nchini kwa maana ya demokrasia na taratibu zake ndani ya mifumo yetu ya uchaguzi.