CCM na Polisi, CHADEMA wanahusikaje?

CCM na Polisi, CHADEMA wanahusikaje?

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
15,835
Reaction score
23,776
Ameandika Malisa GJ kuhusu Mauaji ya Mlelwa wa CCM Njombe

Kwanza kabisa nalaani mauaji ya Bwana Emmanuel Mlelwa kada wa CCM anayedaiwa kuuawa huko Njombe. Either mauaji haya yametokana na sababu za kisiasa au zisizo za kisiasa tunapaswa kukemea kwa nguvu zote. Hakuna sababu yoyote inayo-justify kutoa uhai wa mwenzio. Iwe ya kisiasa au nje ya kisiasa. Hakuna.!

Mpaka sasa watuhumiwa wanne wamekamatwa kwa kuhusishwa na mauaji hayo. Watuhumiwa hao ni Thadeus Mwanyika mgombea udiwani (Chadema) Kata ya Utalingolo, George Sanga mgombea udiwani (Chadema) Kata ya Ramadhani, Optatus Mkwera na Godluck Mfuse ambao ni makada wa Chadema.

Tayari vijana wa CCM wameshaanza kuwahukumu watuhumiwa hao kabla hata mahakama haijaanza kusikiliza kesi. Hii si sawa. Ni mapema mno kuwahukumu watuhumiwa. Wapo watu hutuhumiwa na kukaa mahabusu hata miaka kumi lakini baadae hubainika hawakuhusika.

Polisi wanadai mkanda wa kiunoni wa Mlelwa ulikutwa kwenye gari la Sanga, mgombea udiwani kata ya Ramadhani. Ushahidi huu pekee hautoshi kuhitimisha kwamba Sanga amehusika. Wakazi wa Njombe wanaeleza kuwa mwili wa Mlelwa ulipookotwa ulikua na mkanda. Kwahiyo mkanda uliopatikana kwenye gari ya Sanga sio aliovaa siku alipouawa.

Ukiachana na Sanga ambaye anadaiwa kukutwa na mkanda wa marehemu, watuhumiwa wengine wanashikiliwa kwa sababu simu ya marehemu inaonesha aliwasiliana nao mara ya mwisho kabla hajapotea.

Hata hivyo leo Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Njombe, Rose Mayemba ametoa taarifa kwa vyombo vya habari akieleza kwanini Mlelwa alikua na mawasiliano na watuhumiwa. Kwa mujibu wa Mayemba ni kwamba Mlelwa alikuwa akiwashawishi wagombea udiwani wa Chadema kujitoa kwenye uchaguzi. Tangu alipofika Njombe alikuwa akikutana na wagombea udiwani wa Chadema na kuwashawishi wajitoe.

Mayemba amesema kwamba simu ya Mlelwa kuonekana imewasiliana mara ya mwisho na viongozi wa Chadema sio ushahidi unaotosha kusema kuwa viongozi hao wamemuua. Inawezekana aliuawa na watu wengine ambao hata hakuwasiliana nao kwa simu. Upelelezi utakapokamilika ukweli utajulikana.

Hata hivyo nitoe rai kwa jeshi la polisi kuwa na usawa kunapotokea matukio ya uhalifu yanayohuisha wanasiasa. February mwaka 2018 Katibu wa Chadema kata ya Hananasif Daniel John pamoja na kada mmoja wa Chadema Reginald Mallya walitekwa na watu waliodaiwa kuwa kikundi cha CCM (Green guard) Kinondoni.

Daniel aliuawa kwa kukatwa mapanga na kupasuliwa fuvu. Mallya alifanikiwa kutoroka akiwa amekatwa mapanga usoni na kuvunjwa mkono wa kushoto. Tukio hilo liliripotiwa polisi lakini hakuna yeyote aliyekamatwa, zaidi ya polisi kusema wanafanya upelelezi.

Mwaka huohuo diwani wa Chadema kata ya Namawala huko Kilombero, Godfrey Lwena aliuawa kwa kucharangwa mapanga nyumbani kwake. Kabla ya mauaji hayo Lwena aligombea uenyekiti wa halmashauri ya Kilombero, akidai kushinda lakini matokeo yakapinduliwa na kutangazwa kushindwa kwa kura moja.

Wakati akipigania haki yake ya ushindi ndipo siku moja akiwa nyumbani kwake umeme ukazima majira ya saa 3 usiku. Alipochungulia nyumba za jirani akaona umeme upo. Akaamua kutoka nje aangalie tatizo. Alipofika akakutana na watu wenye mapanga na marungu ambao walimshambulia na kumuua. Polisi kwa haraka wakakemea mauaji hayo kuhusishwa na siasa wakidai huenda ni mauaji ya kisasi.

Mwezi November mwaka jana Mgombea wa Chadema katika nafasi ya Ujumbe wa Serikali ya Mtaa, Sokoni one Arusha (kabla chama hicho hakijajitoa), Cyril Homary aliuawa kwa kuchinjwa shingoni na kitu chenye ncha kali. Cyril alikutwa amefariki nyumbani kwake akiwa na jeraha shingoni na damu nyingi zimetapakaa sakafuni.

Aliyekua Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, ACP Jonathan Shana, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lakini alipiga marufuku kuhusisha tukio hilo na siasa na kutaka watu wasubirie upelelezi polisi. Hata hivyo hakuna mtu yeyote aliyekamatwa hadi sasa.

Matukio haya na mengine ndio yanayoleta ukakasi kwa jeshi la polisi. Ni muhimu jeshi la polisi likawa na usawa kwa matukio yote yanayotokea bila kujali itikadi za kisiasa za mtendwa au mtuhumiwa.

Tunapongeza nguvu kubwa iliyoelekezwa kwa Mlelwa. RPC Njombe ametoa tamko, Mkuu wa upelezi ametoa tamko, Mkuu wa operesheni wa jeshi la polisi ametoa tamko. Ni jambo jema linalotia moyo katika kutafuta haki ya Mlelwa.

Lakini nguvu hiyohiyo ingetumika kwenye mauaji ya Daniel (Hananasif), Lwena (Kilombero), Cyril (Arusha) etc pengine wahusika wangepatikana na kuchukuliwa hatua!

Malisa GJ
 
Kwa mujibu wa polisi huyo kijana aliuwawa na mwanachama wa CHADEMA.

Mimi sina chama ila nimeumia sana, sheria ichukue mkondo wake.

Michango yako mingi unajinasibu huna Chama na hakuna alie kuuliza ,chunga sana Mdomo wako usije ukakuponza unaonekana kabisa Mzani wako unako elemea.
 
Pia sheria ichukue mkondo wake kwa akwilina,Ben saa nane n.k.
sheria isiangalie upande mmoja.
Kwa mujibu wa polisi huyo kijana aliuwawa na mwanachama wa CHADEMA.

Mimi sina chama ila nimeumia sana, sheria ichukue mkondo wake.
 
Kwa mujibu wa polisi huyo kijana aliuwawa na mwanachama wa CHADEMA.

Mimi sina chama ila nimeumia sana, sheria ichukue mkondo wake.
Akina mawazo waliuawa na nani? Polisi wameshughulikiaje suala hilo? Tusitengeneze Taifa lenye Sheria zinazo wahusu baadhi ya watu tu.Hatutakuwa na mwisho mzuri
 
Back
Top Bottom