Mkuu,
Kama kuna chama chenye nafasi ku-turn things around machoni mwa watanzania CCM ndio wana nafasi hiyo.
Wao wanasema wameshika mpini kwa maneno ya Topical. Wao ndio wako kwenye sukani.
Kinachowapasa ni kuifanya serikali kuwa functional sio kama ilivyo sasa.
Kwa mfano, Hivi sasa serikali ina askari polisi wa kuvunja migomo, maandamano ya wanafunzi badala ya kutatua matatizo ya wanafunzi hao.
Serikali ina polisi wengi wa kuzuia mikutano ya upinzani lakini hawana polisi wachache wa kulinda mikutano hiyo.
Serikali inavunja mkataba ambao matokeo yake ni kuilipa kampuni waliyovunja nao mkataba mabilioni ya fedha, badala ya kutatua tatizo la Tanesco. Kuna mapendekezo ya kitaalamu yametolewa humu JF na Mtanganyika kwenye thread ya CHADEMA kuandamana kupinga kupanda bei ya umeme. Hii ni mifani michache tu.
Hawawezi kuendelea kumuomba mlalahoi akaze mkanda wakati wao wanatanua tu.
Sijui nani ni mshauri wa CCM na serikali yake lakini between now hadi 2015 wanaweza kuchapa kazi kama wako makini na 2015 wananchi watakipigia kura na kubakia madarakani bila ya kuchakachua. Wana ujasiri huo?
Kuna mama mmoja alishasema kuwa katika CCM hakuna msafi, lakini watanzania hawahitaji malaika , wanachohitaji ni mzalendo mwenye uchungu na nchi na rasilimali zake kwa manufaa ya wote.
Nini wafanye.?
Washughulikie wala rushwa vigogo sio vidagaa tu.
Wapige vita ufisadi kwa vitendo sio domo tupu majukwaani.
Wapeleke huduma za jamii vijijini.
Serikali iache matumizi ya anasa kama ununuzi wa VX
Wakati huo huo walete Katiba mpya
Rais Kikwete anaweza kuibuka "a hero" at the end of his term.
Siku nyengine nitatoa ushauri wangu vipi wanaweza kupiga vita rushwa, vipi wanaweza kushughulikia fisadis hata kama viongozi ni miongoni mwao. I will suggest a very human way, isiyo ya kukomoa ,wala kulipa visasi and very practical.
Ninaiandaa. Kwa hiyo CCM wasome JF wapate Ideas.
Sisi wengine ni raia wema si washabiki wa chama chochote cha siasa na tunaitakia mema nchi yetu. Lakini right now tunaona kama nchi imepoteza muelekeo.